WhatsApp hushiriki taarifa zipi na Kampuni za Meta?

Kwa sasa WhatsApp inashiriki aina fulani ya taarifa na Kampuni za Meta. Taarifa tunazoshiriki na Kampuni nyingine za Meta zinajumuisha taarifa za usajili wa akaunti yako (kama vile nambari yako ya simu), data ya muamala (kwa mfano, ukitumia Facebook Pay au Maduka katika WhatsApp), taarifa zinazohusiana na huduma, taarifa kuhusu jinsi unavyotangamana na biashara unapotumia Huduma zetu, taarifa za kifaa cha mkononi, anwani yako ya IP, na inaweza kujumuisha taarifa nyingine iliyobainishwa katika sehemu ya Sera ya Faragha yenye kichwa ‘Taarifa Tunazokusanya’ au tulizopata baada ya kukuarifu au kutokana na kibali chako.
Tunadhibiti taarifa tunayoshiriki na Meta katika njia muhimu. Kwa mfano, kila wakati, tutalinda mazungumzo yako ya binafsi kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, hivi kwamba WhatsApp wala Meta haziwezi kuona ujumbe wako wa faragha. Hatuweki kumbukumbu za kila mtu anayetuma ujumbe au kupiga simu na hatuwezi kuona eneo lako lililoshirikiwa kwa hivyo hatuwezi na hatushiriki hili na Meta. Tunahitaji anwani zako ili kutoa huduma, lakini hatushiriki anwani zako na Meta. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu baadhi ya vikwazo hivi hapa.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La