"Kikundi hiki hakipatikani tena" inamaanisha nini?

WhatsApp inadumisha teknolojia mahiri ya mashine kujifunza ili kutathmini taarifa za vikundi ikiwa ni pamoja na mada ya vikundi, picha za jalada na maelezo ya vikundi. Vilevile, tunatoa chaguo rahisi kwa watumiaji kutuma ripoti kwetu kutoka kwenye soga yoyote. Tunaweza kuzuia shughuli zaidi katika vikundi vya soga ili kutii wajibu wetu wa kisheria au wakati msimamizi wa kikundi anakiuka Masharti yetu ya Huduma.
Kwa usaidizi wa ziada, tafadhali wasiliana na timu yetu ya Msaada wa WhatsApp.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La