Kuhusu ujumbe unaotoweka

Ujumbe unaotoweka ni kipengele cha hiari ambacho unaweza kukiwasha kwa ajili ya faragha zaidi.
Unapowasha ujumbe unaotoweka, unaweza kuweka ujumbe utoweke baada ya saa 24, siku 7 au siku 90 baada ya muda ulipotumwa. Uteuzi wa hivi karibuni unadhibiti tu ujumbe mpya kwenye soga. Unaweza kuchagua kuwasha ujumbe unaotoweka kwa soga zako zote, au uchague soga mahususi. Mipangilio hii haitaathiri ujumbe wa awali ulioutumwa au kupokelewa kwenye soga. Katika soga ya binafsi, wewe au mwenzio mnaweza kuwasha au kuzima hali ya ujumbe unaotoweka. Kwenye soga ya kikundi, washiriki wowote wa kikundi wanaweza kuwasha au kuzima ujumbe unaotoweka. Hata hivyo, msimamizi wa kikundi anaweza kubadilisha mipangilio ya kikundi kuruhusu wasimamizi tu kuwasha au kuzima ujumbe unaotoweka.
  • Mtumiaji asipofungua WhatsApp ndani ya saa 24, siku 7 au siku 90, ujumbe utatoweka kwenye soga. Hata hivyo, onyesho tangulizi la ujumbe bado linaweza kuonekana kwenye taarifa mpaka WhatsApp itakapofunguliwa.
  • Unapojibu ujumbe, ujumbe wa awali unanukuliwa. Ukijibu ujumbe unaotoweka, ujumbe ulionukuliwa unaweza kubakia kwenye soga baada ya muda uliochagua.
  • Ujumbe unaotoweka ukisambazwa kwenye soga isiyo na ujumbe unaotoweka, ujumbe hautatoweka kwenye soga iliyosambazwa.
  • Mtumiaji akihifadhi nakala ya soga kabla ya ujumbe kutoweka, ujumbe unaotoweka utajumuishwa kwenye nakala rudufu. Ujumbe unaotoweka utafutwa mtumiaji atakaporejesha kutoka kwenye nakala rudufu.
Kumbuka: Tumia ujumbe unaotoweka na watu wanaoaminika tu. Kwa mfano, inawezekana kwa mtu fulani:
  • Kusambaza au kupiga picha ya skrini ya ujumbe unaotoweka na kuuhifadhi kabla haujatoweka.
  • Kunakili na kuhifadhi maudhui kutoka kwenye ujumbe unaotoweka kabla haujatoweka.
  • Kupiga picha ujumbe unaotoweka kwa kamera au vifaa vingine kabla haujatoweka.
Ujumbe unaotoweka kwa akaunti yako
Unaweza kuwasha ujumbe unaotoweka kwa chaguomsingi katika soga zote mpya binafsi.
  • iPhone na Android: Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp > Faragha > Muda chaguomsingi wa ujumbe kisha uchague urefu wa muda.
Maudhui katika ujumbe unaotoweka
Kwa kawaida, maudhui yanayopakuliwa kwenye WhatsApp yatapakuliwa kiotomatiki kwenye picha zako. Kama umewasha hali ya ujumbe unaotoweka, maudhui yanayotumwa kwenye soga yatatoweka, lakini yatahifadhiwa kwenye simu kama umewasha hali ya kupakua kiotomatiki. Unaweza kuzima pakua kiotomatiki kwenye WhatsApp Mipangilio > Hifadhi na Data.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La