Jinsi ya kuongeza anwani
Kuna njia kadhaa za kuongeza anwani.
Kuongeza anwani kwa soga mpya
- Fungua WhatsApp.
- Nenda kwenye kichupo cha Soga.
- Gusa Soga mpya> Anwani mpya.
Kuongeza kutoka kwenye soga (namba ambazo hazijahifadhiwa ambazo umepiga nazo soga)
- Fungua WhatsApp.
- Nenda kwenye kichupo cha Soga.
- Chagua soga na mtumiaji ambaye hajahifadhiwa. Itawakilishwa na namba badala ya jina katika Orodha ya Soga.
- Gusa upau wa juu wa programu ili uone Maelezo ya Soga.
- GusaUnda Anwani Mpya.
Kuongeza kutoka kwenye vikundi
- Gusa ujumbe kutoka kwa mtu asiye kwenye anwani zako.
- Gusa Ongeza kwenye anwani. Chagua mojawapo ya:
- Unda Anwani Mpya - Thibitisha jina na namba ya simu.
- Ongeza kwa Anwani Iliyopo - Chagua anwani iliyopo na uthibitishe jina na namba ya simu.
Kuongeza watumiaji walio na namba za simu za kimataifa, soma makala haya.