Kuzuiwa na mtu

Kuna ishara kadhaa za kuonyesha kwamba unaweza kuwa umezuiwa:
  • Huoni tena mara ya mwisho mtumiaji alipokuwa mtandaoni au kwamba yupo mtandaoni katika soga. Pata maelezo hapa.
  • Huoni masasisho ya picha ya jalada ya mtumiaji.
  • Ujumbe wowote unaotuma kwa mtumiaji ambaye amekuzuia utaonyesha alama moja ya tiki (ujumbe umetumwa), na hauwezi kuonyesha ya pili ya tiki (ujumbe umewasilishwa).
  • Simu zozote unazojaribu kupiga hazitafanikiwa.
Ukishuhudia ishara hizi zote, inaweza kumaanisha kuwa mtumiaji huyo amekuzuia. Hata hivyo, kuna uwezekano mwingine. Tumefanya hili kutokuwa bayana kimakusudi ili kulinda faragha yako unapomzuia mtu. Kwa hiyo, hatuwezi kusema kama umezuiwa na mtu mwingine.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kumzuia mtu kwenye: Android | iPhone
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La