Â
Jinsi ya kuangalia taarifa za kusomwa
Android
iPhone
KaiOS
Alama za tiki zitaonekana karibu na kila ujumbe utakaotuma. Kila moja inaashiria yafuatayo:
- Ujumbe umetumwa.
- Ujumbe uliwasilishwa kwenye simu ya mpokeaji au vifaa vyake vinginevyo vilivyounganishwa.
- Mpokeaji amesoma ujumbe.
Kumbuka:
- Alama ya tiki ya pili itaonekana wakati ujumbe umewasilishwa kwenye kifaa chochote cha mpokeaji kilichounganishwa, hata kama simu yake imezimwa.
- Katika soga ya kikundi, alama ya tiki ya pili huonekana wakati washiriki wote katika kikundi wamepokea ujumbe wako. Alama za tiki mbili za bluu huonekana wakati washiriki wote katika kikundi wameusoma ujumbe wako.
Maelezo ya ujumbe
Kwa ujumbe wowote unaoutuma, utaweza kuona skrini ya maelezo ya ujumbe, inayoonyesha maelezo ya wakati ujumbe wako uliwasilishwa, kusomwa au kuchezwa na mpokeaji.
Kuona skrini ya maelezo ya ujumbe:
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa na ushikilie ujumbe ulioutuma.
- Gusa . Au, unaweza kugusa Chaguo zaidi> Maelezo.
Skrini ya maelezo ya ujumbe huonyesha:
Umewasilishwa:
- Ujumbe wako umewasilishwa kwenye simu au vifaa vya mpokeaji vilivyounganishwa lakini mpokeaji hajauona.
Umesomwa au Umeonwa:
- Mpokeaji amesoma ujumbe wako au kuona picha yako, faili ya sauti au video.
- Mpokeaji ameona ujumbe wako wa sauti, lakini hajaucheza.
Umechezwa:
- Mpokeaji amecheza ujumbe wako wa sauti.
Kumbuka: Mshiriki anapoondoka kwenye kikundi, skrini ya Maelezo ya ujumbe bado itaonyesha maelezo ya awali ikiwa na washiriki wote, ikiwa ni pamoja na mshiriki ambaye ameondoka kwenye kikundi.
Kukosa taarifa za kusomwa
Ikiwa huoni alama mbili za tiki za bluu, kipaza sauti cha bluu au maandishi "Imefunguliwa" karibu na ujumbe wako uliotumwa au ujumbe wa sauti:
- Inawezekana kuwa wewe au mpokeaji mmezima taarifa za kusomwa kwenye mipangilio ya faragha.
- Inawezekana mpokeaji amekuzuia.
- Inawezekana mpokeaji hajafungua mazungumzo yenu.
- Inawezekana wewe au mpokeaji mna matatizo ya muunganisho.
Kuzima taarifa za kusomwa
Kuzima taarifa zako za kusomwa, gusa Chaguo zaidi
> Mipangilio > Faragha kisha uzime Taarifa za kusomwa.

Kumbuka: Hatua hii haiwezi kuzima taarifa za kusomwa za soga za kikundi au taarifa za kucheza kwa ujumbe wa sauti. Hakuna njia ya kuzima mipangilio hiyo.