Jinsi ya kupakua programu ya WhatsApp Business

Android
iOS
Programu ya WhatsApp Business ni programu inayoweza kupakuliwa bila malipo kwa ajili ya biashara ndogo.
Kabla ya kupakua programu, tafadhali fahamu yafuatayo:
 • Ikiwa una akaunti ya WhatsApp Messenger, unaweza kuhamisha akaunti yako kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na historia ya soga na maudhui, kwenda kwenye akaunti mpya ya WhatsApp Business.
 • Historia yako ya soga haiwezi kurudishwa kwenye WhatsApp Messenger ikiwa utaamua kuacha kutumia programu ya WhatsApp Business.
 • Unaweza kutumia WhatsApp Business na WhatsApp Messenger kwa wakati mmoja, lakini ni lazima uunganishe akaunti hizo ukitumia namba tofauti za simu. Haiwezekani kuwa na namba moja ya simu inayohusishwa na programu zote mbili kwa wakati mmoja.

Ili kuweka mipangilio ya programu ya WhatsApp Business:

 1. Pakua programu ya WhatsApp Business kwenye Duka la Google Play.
 2. Thibitisha namba yako ya simu ya biashara.
 3. Rejesha akaunti yako kutoka kwenye hifadhi ya nakala, ikiwa ungependa kufanya hivyo.
 4. Weka jina lako la biashara.
 5. Unda jalada lako. Gusa Chaguo zaidi
  more options
  > Mipangilio > jina la biashara yako.

Rasilimali zinazohusiana:

Je, hili linajibu swali lako?

Ndiyo
La