Jinsi ya kupakua programu ya WhatsApp Business

Android
iOS
Kumbuka: Maelezo katika makala haya yanalenga biashara zinazotumia programu ya WhatsApp Business. Biashara zinazotafuta hali bora ya utumiaji wa ujumbe wa biashara zinafaa kuzingatia kutumia Jukwaa la WhatsApp Business. Ili upate maelezo zaidi kuhusu suluhu tofauti za kutuma ujumbe wa biashara ambazo WhatsApp inatoa, angalia makala haya.
Programu ya WhatsApp Business ni programu inayoweza kupakuliwa bila malipo kwa ajili ya biashara ndogo.
Kabla ya kupakua programu, tafadhali fahamu yafuatayo:
  • Ikiwa una akaunti ya WhatsApp Messenger, unaweza kuhamisha akaunti yako kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na historia ya soga na maudhui, kwenda kwenye akaunti mpya ya WhatsApp Business.
  • Ukiamua kuacha kutumia programu ya WhatsApp Business, unaweza kuhamisha akaunti yako na historia ya soga kurudi kwenye WhatsApp Messenger.
  • Unaweza kutumia WhatsApp Business na WhatsApp Messenger kwa wakati mmoja, lakini ni lazima uunganishe akaunti hizo ukitumia namba tofauti za simu. Haiwezekani kuwa na namba moja ya simu inayohusishwa na programu zote mbili kwa wakati mmoja.

Anza

  1. Pakua programu ya WhatsApp Business kwenye Duka la Google Play.
  2. Fungua programu ya WhatsApp Business.
  3. Kagua Masharti ya Huduma ya WhatsApp Business . Ili ukubali, gusa Kubali na uendelee.
  4. Thibitisha namba yako ya simu.
WhatsApp itatafuta nakala zozote zinazohusiana na namba yako ya simu. Ikiipata, unaweza kurejesha historia yako ya soga.
Ikiwa wewe ni mgeni kwenye programu ya WhatsApp Business au ikiwa huwezi kurejesha nakala, programu ya WhatsApp Business itakuongoza katika mchakato wa kuunda jalada la biashara.

Kuunda jalada la biashara

  1. Weka jina la biashara. Gusa Inayofuata.
  2. Chagua hadi aina tatu za biashara. Unaweza kuchagua kati ya aina zilizopendekezwa au uguse + Angalia aina zaidi ili ugundue chaguo zingine. Gusa Inayofuata.
    • Kumbuka: Huwezi kuunda aina maalum ya biashara.
  3. Kuweka saa zako za kazi. Gusa Inayofuata.
  4. Kuweka picha ya jalada. Gusa Inayofuata au uguse Ruka ili ufanye kitendo hiki baadaye.
  5. Kuweka anwani ya biashara na kiungo cha tovuti ya biashara yako ili kuwasaidia wateja kukupata. Gusa Inayofuata au uguse Ruka ili ufanye kitendo hiki baadaye.
  6. Kuweka maelezo ya biashara ili kuwaambia wateja watarajiwa kuhusu biashara yako. Gusa Inayofuata au uguse Ruka ili ufanye kitendo hiki baadaye.
  7. Ukimaliza, gusa Nimemaliza.
Kuandika maelezo ya biashara ukitumia msaada wa Meta AI
Ili utumie Meta AI kukusaidia kuboresha maelezo ya biashara yako:
  1. Weka rasimu ya maelezo ya biashara yako.
  2. Gusa
    Boresha ukitumia Meta AI.
Meta AI itaunda orodha ya maelezo ya biashara inayotarajiwa.
Chagua unachopenda kisha uguse Inayofuata au uguse
Andika maelezo mapya ili ugundue chaguo zingine. Unaweza kuhariri maelezo ya biashara yanayoandikwa na Meta AI kila wakati.

Kukamilisha

  1. Gusa Unda ufunguo wa siri ili kurahisisha kuingia katika akaunti au uguse Ruka ili kufanya kitendo hiki baadaye.
  2. Gusa Weka barua pepe ili uweke anwani ya barua pepe ili kukusaidia kufikia akaunti yako au uguse Ruka ili ufanye kitendo hiki baadaye.

Hatua zinazofuata

Je, hili linajibu swali lako?

Ndiyo
La