Jinsi ya kuhariri jalada lako la biashara

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Android
iPhone
Jalada lako la biashara linakuruhusu kuongeza maelezo kuhusu kampuni yako, ikiwa ni pamoja na jina la biashara yako, anwani, aina, maelezo, anwani ya barua pepe na tovuti. Watu wanaweza kuona maelezo haya kwa urahisi wanapoangalia jalada lako.
Ili uangalie jalada la biashara yako, fungua programu ya WhatsApp Business. Kisha, gusa Mipangilio > Zana za Biashara > Jalada la Biashara.
Kuhariri picha yako ya jalada
 1. Gusa Hariri chini ya picha ya jalada lako.
  • Kumbuka: Ikiwa hujaweka picha ya jalada, gusa Weka Picha badala yake.
 2. Gusa Chagua Picha ili uchague picha iliyopo au Piga Picha ili kupiga picha mpya. Unaweza pia kugusa Futa Picha > Futa Picha ili kuondoa picha yako ya sasa ya jalada.
 3. Baada ya kuchagua picha au kupiga mpya, punguza au zungusha picha unavyotaka.
 4. Gusa Chagua.
Kumbuka: Picha yako ya jalada inaonekana hadharani kwa chaguomsingi. Pata maelezo ya jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha kwenye makala haya.
Kuhariri picha yako ya jalada
 1. Gusa Kamera
  kwenye picha ya jalada lako.
 2. Gusa Chagua Picha ili uchague picha iliyopo au Piga Picha ili kupiga picha mpya. Unaweza pia kugusa Futa Picha > Futa Picha ili kuondoa picha yako ya sasa.
 3. Baada ya kuchagua picha au kupiga mpya, punguza au zungusha picha unavyotaka.
 4. Gusa Chagua.
Kumbuka: Picha yako ya wasifu inaonekana hadharani kwa chaguomsingi.
Kuhariri jina na maelezo ya biashara yako
 1. Gusa sehemu ambayo ungependa kusasisha.
 2. Fanya masasisho yako.
 3. Gusa Hifadhi.
Kuhariri namba yako ya simu
Soma makala haya ili ufahamu jinsi ya kuhariri namba yako ya simu.
Kuhariri saa za kazi za biashara yako
 1. Gusa sehemu ya Weka Saa za Biashara.
 2. Chini ya RATIBA, chagua moja ya vielelezo vya ratiba vifuatavyo:
  • Imefunguliwa kwa saa maalum: Gusa siku ili ubadilishe saa zako za kazi kwa siku hiyo.
  • Imefunguliwa kila wakati: Tumia kigeuzi hiki ili kuchagua siku za juma ambapo biashara yako imefunguliwa.
  • Kwa miadi tu: Tumia kigeuzi hiki ili kuchagua siku za juma ambapo biashara yako imefunguliwa kupokea miadi.
 3. Gusa Hifadhi.
Unaweza pia kugusa Futa ili kuweka upya saa zako za kazi.
Kuhariri anwani ya biashara yako
 1. Gusa sehemu ya Weka Anwani.
 2. Weka anwani ya biashara yako.
 3. Unaweza pia kusasisha eneo lako kwenye ramani kwa kuwasha Weka mahali kwenye ramani.
 4. Kisha, sasisha anwani ya biashara yako kwenye ramani au chagua mojawapo ya zifuatazo:
  • Ndiyo, Tumia Anwani Hii ili ramani ionyeshe ulichoweka katika sehemu ya anwani.
  • Hapana, Hariri Anwani ili kurudi katika sehemu ya anwani ya biashara halafu ubadilishe anwani yako.
  • Acha Niweke Mahali ili kutafuta mahali maalumu kwenye ramani.
 5. Gusa Nimemaliza.
  • Kumbuka: Kufanya hivi kunabadilisha tu eneo la biashara yako kwenye ramani. Anwani uliyoweka katika sehemu ya anwani itabaki ilivyo.
 6. Gusa Hifadhi.
Ili kuondoa anwani yako, gusa Futa Anwani.
Kuhariri anwani yako ya barua pepe na tovuti
 1. Gusa sehemu ambayo ungependa kusasisha.
 2. Sasisha taarifa zako.
 3. Gusa Hifadhi.
Kuhariri katalogi yako
 1. Gusa DHIBITI ili kusasisha katalogi yako au kuunda mpya.
 2. Ongeza au hariri vitu kwenye katalogi yako unavyotaka. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi kwenye makala haya.
Kuhariri akaunti zako za mitandao ya kijamii ulizounganisha
Ikiwa huna akaunti ulizounganisha:
 1. Gusa Ongeza Akaunti ili kuunganisha akaunti ya mtandao wa kijamii.
 2. Gusa Facebook au Instagram > Endelea.
 3. Ingia kwenye akaunti yako ya Facebook au Instagram ili uiweke kwenye jalada lako la biashara.
Ikiwa tayari una akaunti zilizounganishwa:
 1. Gusa Facebook au Instagram ili kudhibiti akaunti yako iliyounganishwa.
 2. Unaweza kuficha akaunti iliyounganishwa kutokea kwa jalada lako kwa kuzima Onyesha kwenye jalada au kuitenganisha na jalada lako la biashara kwa kugusa Ondoa WhatsApp.
Kuhariri aina ya biashara yako
 1. Gusa sehemu ya aina.
 2. Chagua hadi aina tatu zinazofaa kwa ajili ya biashara yako.
 3. Gusa Hifadhi.
Kuhariri taarifa zilizo katika sehemu ya "Kuhusu"
 1. Gusa sehemu ya Kuhusu.
 2. Unaweza kugusa sehemu iliyo chini ya KWA SASA IMEWEKWA ili kuunda ujumbe maalumu wa Kuhusu au chagua mojawapo ya maelezo yaliyowekwa mapema katika sehemu ya CHAGUA KUHUSU.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La