Â
Jinsi ya kuhariri jalada lako la biashara
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Android
iPhone
Jalada lako la biashara linakuruhusu kuongeza maelezo kuhusu kampuni yako, ikiwa ni pamoja na jina la biashara yako, anwani, aina, maelezo, anwani ya barua pepe na tovuti. Watu wanaweza kuona maelezo haya kwa urahisi wanapoangalia jalada lako.
Kidokezo cha Biashara: Jalada kamili na sahihi la biashara haliwafahamishi tu wateja wako. Pia linaweza kupunguza idadi ya ujumbe unaopokea kuhusu mambo kama vile saa zako za kazi.
Ili uangalie jalada la biashara yako, fungua programu ya WhatsApp Business. Kisha, uguse Chaguo zaidi
> Zana za biashara > Jalada la Biashara.

Kuhariri picha yako ya jalada
- Gusa picha ya jalada lako, kisha uguse Hariri.
- Au uguse Haririkwenye picha ya jalada lako, kisha uguse Weka au badilisha picha ya jalada.
- Gusa Kamera ili upige picha mpya au uguse Matunzio ili uchague picha iliyopo. Unaweza pia kugusa Futa> ONDOA ili kuondoa picha yako ya sasa ya jalada.
- Baada ya kuchagua picha au kupiga mpya, punguza au zungusha picha unavyotaka.
- Gusa NIMEMALIZA.
Kumbuka: Picha yako ya jalada itaonekana hadharani kwa chaguomsingi. Pata maelezo zaidi ya jinsi ya kubadilisha mipangilio yako ya faragha kwenye makala haya.
Kuhariri picha yako ya jalada
- Gusa Haririkwenye picha ya jalada lako.
- Gusa Weka au hariri picha ya jalada.
- Gusa Kamera ili kupiga picha mpya au uguse Matunzio ili kuchagua picha iliyopo. Pia unaweza kugusa Futa> ONDOA ili kuondoa picha yako ya sasa ya jalada.
- Baada ya kuchagua picha au kupiga mpya, punguza au zungusha picha unavyotaka.
- Gusa NIMEMALIZA.
Kumbuka: Picha yako ya jalada inaonekana hadharani kwa chaguomsingi.
Kuhariri jina na maelezo ya biashara yako
- Gusa Haririkatika sehemu ambayo ungependa kusasisha.
- Fanya masasisho yako.
- Gusa SAWA au HIFADHI.
Kuhariri aina ya biashara yako
- Gusa Haririkwenye sehemu ya aina.
- Chagua hadi aina tatu zinazofaa kwa ajili ya biashara yako.
Kuhariri anwani ya biashara yako
- Gusa Haririkwenye sehemu ya anwani.
- Gusa sehemu ya Anwani ya biashara, kisha uweke anwani yako ya biashara.
- Unaweza pia kusasisha mahali ulipo kwenye ramani kwa kugusa WEKA MAHALI KWENYE RAMANI au SASISHA MAHALI KWENYE RAMANI. Sasisha anwani yako ya biashara kwenye ramani, kisha uguse NIMEMALIZA.
Kumbuka: Hii inabadili tu mahali pa biashara yako kwenye ramani. Anwani uliyoweka kwenye sehemu ya anwani haitabadilika.
- Gusa HIFADHI.
Kuhariri saa za kazi za biashara yako
- Gusa Haririkwenye sehemu ya saa za kazi.
- Gusa Ratiba.
- Chagua mojawapo ya vielelezo vya ratiba vifuatavyo:
- Imefunguliwa kwa saa maalum: Tumia kigeuzi hiki ili kuchagua siku mahususi ambazo umefungua. Unaweza pia kuonyesha vikundi vya saa maalumu za kazi kwa kila siku.
- Imefunguliwa kila wakati: Tumia kigeuzi hiki ili kuchagua siku za juma ambapo biashara yako imefunguliwa.
- Kwa miadi tu: Tumia kigeuzi hiki ili kuchagua siku za juma ambapo biashara yako imefunguliwa kupokea miadi.
- Gusa HIFADHI.
Unaweza pia kugusa Chaguo zaidi
> Futa ili kubadili saa zako za kazi.

Kuhariri anwani yako ya barua pepe na tovuti
- Gusa Haririkwenye sehemu ambayo ungependa kusasisha.
- Sasisha taarifa zako.
- Gusa HIFADHI.
Kuhariri akaunti zako za mitandao ya kijamii ulizounganisha
Ikiwa huna akaunti ulizounganisha:
- Gusa Weka Facebook au Instagram.
- Gusa Facebook au Instagram > ENDELEA.
- Ingia kwenye akaunti yako ili uiweke kwenye jalada la biashara yako.
Ikiwa tayari una akaunti zilizounganishwa:
- Gusa Haririkaribu na jina la ukurasa wako wa Facebook au Instagram ili udhibiti akaunti iliyounganishwa.
- Unaweza kuficha akaunti iliyounganishwa kutokea kwenye jalada lako au kuitenganisha kutokea kwenye akaunti yako ya WhatsApp.
Kuhariri katalogi yako
- Gusa DHIBITI ili kusasisha katalogi yako au kuunda mpya.
- Ongeza au hariri vitu kwenye katalogi yako unavyotaka. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuunda na kudumisha katalogi kwenye makala haya.
Kuhariri taarifa zilizo katika sehemu ya "Kukuhusu"
- Gusa Haririkwenye sehemu ya Kuhusu.
- Unaweza kuunda ujumbe maalum wa Kuhusu au uchague moja ya zilizowekwa awali kwenye sehemu ya Chagua Kuhusu.
Kuhariri namba yako ya simu
Gusa Hariri
kwenye sehemu ya namba ya simu > INAYOFUATA ili kuanza mchakato wa kusasisha namba yako ya simu.

Rasilimali zinazohusiana:
- Kuhusu jalada la biashara yako
- Jinsi ya kuhariri jalada la biashara yako: iPhone | Web na Desktop