Kuhusu kuhama kati ya WhatsApp Messenger na programu ya WhatsApp Business

WhatsApp Messenger na WhatsApp Business ni programu mbili tofauti. Huwezi kutumia namba ile ile ya simu kwenye programu zote mbili kwa wakati mmoja, lakini inawezekana kuhama kutoka programu moja kwenda kwenye nyingine.
Kuhamisha taarifa za akaunti yako kutoka kwenye WhatsApp Messenger hadi katika programu ya WhatsApp Business ni rahisi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutoka kwenye WhatsApp Messenger kwenda katika WhatsApp Business kwenye Android na iPhone.
Pia inawezekana kutoka kwenye programu ya WhatsApp Business kwenda kwenye WhatsApp Messenger. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutoka kwenye programu ya WhatsApp Business kwenda katika WhatsApp Messenger kwenye Android na iPhone.
Kumbuka: Ingawa inawezekana kuhamisha baadhi ya maelezo ya akaunti yako kutoka programu ya WhatsApp Business hadi kwenye WhatsApp Messenger, vipengele vya programu ya WhatsApp Business havitahamia kwenye WhatsApp Messenger. Hii ina maana kuwa maelezo ya akaunti yanayohusiana na vipengele vya kipekee vya programu ya WhatsApp Business, kama vile bidhaa za katalogi na mikusanyiko, haviwezi kuhamishwa.
Rasilimali zinazohusiana:
Kuhusu programu ya WhatsApp Business
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La