Jinsi ya kubadilisha mandhari yako

WhatsApp inakuruhusu kubinafsisha soga zako kwa kubadilisha mandhari yako. Unaweza kubadilisha mandhari yako kwa soga zote au kuweka mandhari kwa soga maalumu. Unaweza pia kuchagua soga maalumu kwa kuweka hali ya giza au mwanga na kufifiza hali ya giza ya mandhari yako.
Badilisha mandhari kwa soga zote
 1. Gusa Hiari zaidi
  > Mipangilio > Soga > Mandhari.
  • Mbadala, unaweza kufungua soga > gusa Hiari zaidi
   > Mandhari.
  • Kama unatumia hali ya giza, unaweza kutumia kitelezi ili kufifiza mandhari yako ya sasa.
 2. Gusa BADILISHA.
 3. Chagua aina ya mandhari, kisha chagua picha unayotaka kuiweka kama mandhari yako.
  • Unaweza pia kugusa Mandhari ya kawaida kurejesha mandhari ya kawaida ya WhatsApp.
 4. Gusa WEKA MANDHARI.
Badilisha mandhari kwa soga maalumu
 1. Fungua soga unayotaka kuibadilishia mandhari.
 2. Gusa Hiari zaidi
  > Mandhari.
  • Kama unatumia hali ya giza, unaweza kutumia kitelezi ili kufifiza mandhari yako ya sasa.
 3. Chagua aina ya mandhari, kisha chagua picha unayotaka kuiweka kama mandhari yako.
  • Unaweza pia kugusa Mandhari ya chaguo msingi kurejesha mandhari ya chaguo msingi ya WhatsApp.
 4. Gusa WEKA MANDHARI.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La