Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Mac
Ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp hukuruhusu kuwasiliana papo hapo na anwani na vikundi. Unaweza kuutumia kuwasilisha taarifa muhimu na za haraka. Ujumbe wote wa sauti hupakuliwa kiotomatiki.
Pia unaweza kurekodi, kuhakiki na kurekodi upya masasisho ya hali kabla ya kuyashiriki kwa watu uliowachagua. Wapokeaji wako wanaweza kusikiliza sasisho lako na kuangalia picha inayoendelea wakati sauti inacheza.
Kutuma ujumbe wa sauti
 1. Fungua soga ambayo ungependa kuitumia ujumbe wa sauti.
 2. Bonyeza na ushikilie
  iliyo karibu na sehemu ya kuandikia, kisha uanze kuzungumza. Unaweza pia kutelezesha kidole juu ili kurekodi bila kushikilia. Kumbuka: ikiwa utaona
  badala yake, gusa aikoni hiyo ili ubadilishe kwenda
  .
 3. Unapomaliza, ondoa kidole chako kwenye
  ili utume ujumbe wako kiotomatiki. Au ikiwa unarekodi bila kushikilia, gusa
  ili usitishe kurekodi na uhakiki rasimu ya ujumbe wako kabla ya kuutuma. Gusa
  ili uendelee kurekodi.
Kumbuka:
 • Unaporekodi unaweza kutelezesha
  ili ughairi na ufute ujumbe wako wa sauti.
 • Ikiwa mwanzo wa ujumbe wako haujarekodiwa, huenda ukahitaji kusubiri sekunde moja kabla ya kuanza kuzungumza.
Kwenye ujumbe wa sauti ambao umetuma
 • huonyesha kwamba wapokeaji wote hawajacheza ujumbe, lakini huenda baadhi wamecheza.
 • huonyesha kuwa wapokeaji wote wamecheza ujumbe.
Kurekodi na kutuma sasisho la hali la sauti
Unaweza kurekodi na kutuma hali ya sauti yenye urefu wa hadi sekunde 30.
 1. Gusa kichupo cha Masasisho.
 2. Gusa
  > aikoni ya penseli.
 3. Bonyeza na ushikilie
  , kisha uanze kuzungumza.
 4. Unapomaliza, ondoa kidole chako kwenye
  .
 5. Chagua soga ya anwani au ya kikundi ambayo ungependa kushiriki sasisho lako nayo.
 6. Gusa
  ili utume hali yako ya sauti.
Kumbuka: Ikiwa mwanzo wa ujumbe wako haujarekodiwa, huenda ukahitaji kusubiri sekunde moja kabla ya kuanza kuzungumza.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La