Â
Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti
Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp hukuruhusu kuwasiliana papo hapo na watu pamoja na vikundi. Unaweza kuutumia kuwasilisha taarifa muhimu na za haraka. Ujumbe wote wa sauti hupakuliwa kiotomatiki.
Unaweza pia kurekodi na kushiriki masasisho ya sauti kwenye hali.
Unaweza kuhakiki sasisho la hali kabla ya kulituma na kulirekodi tena ikiwa unahitaji. Kisha, ushiriki sasisho lako na anwani ulizochagua. Zitaweza kusikiliza sasisho lako na kuona picha inayoendelea sauti inapocheza.
Kutuma ujumbe wa sauti
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa na ushikilie maikrofonikisha uanze kuzungumza.
- Ukimaliza, ondoa kidole chako kwenye maikrofoni. Ujumbe wa sauti utatumwa kiotomatiki.


Unaporekodi ujumbe wa sauti, unaweza telezesha kidole ili kughairi
.



Kurekodi ujumbe mrefu wa sauti
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Gusa na ushikilie maikrofonikisha uanze kuzungumza.
- Telezesha kidole juu ili uanze kurekodi bila kushikilia.
- Ukimaliza, gusa Tumaili utume ujumbe.
Unaporekodi ujumbe mrefu wa sauti, unaweza kugusa Ghairi ili ughairi. Unaweza pia kugusa kitufe chekundu cha kusitisha
ili usitishe kunakili au uhakiki rasimu ya ujumbe wako. Gusa aikoni nyekundu ya maikrofoni
ili kuendelea kunakili kwenye ujumbe huo huo wa sauti.


Kurekodi na kutuma sasisho la hali la sauti
Unaweza kurekodi na kushiriki masasisho ya sauti ya hadi sekunde 30.
- Fungua kichupo chako cha Hali.
- Teua chaguo la maandishi .
- Kwenye kiundaji cha maandishi, gusa na ushikilie maikrofoni kisha uanze kuzungumza.
- Ukimaliza, ondoa kidole chako kwenye maikrofoni . Chagua anwani au soga ya kikundi unayotaka kushiriki sasisho lako.
- Gusa .
Kumbuka: Kwenye baadhi ya simu, unaweza kusubiri kwa sekunde moja kabla ya kuzungumza ikiwa mwanzo wa ujumbe wako haukurekodiwa.
Kwenye ujumbe wa sauti uliotumwa utaona:
- Maikrofoni ya kijivu kwa ujumbe wa sauti ambao haujachezwa na wapokeaji wote (lakini unaweza kuwa umechezwa na baadhi).
- Maikrofoni ya bluu kwa ujumbe wa sauti ambao wapokeaji wote wameucheza.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kucheza ujumbe wa sauti
- Jinsi ya kuhakiki ujumbe wa sauti