Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Ujumbe wa sauti kwenye WhatsApp hukuruhusu kuwasiliana papo hapo na waasiliani na vikundi. Unaweza kuutumia kuwasilisha taarifa muhimu na za haraka. Kwa hivyo, ujumbe wote wa sauti hupakuliwa kiotomatiki.
Kutuma ujumbe wa sauti
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Bofya maikrofoni
  na uanze kuzungumza.
 3. Mara ukimaliza, bofya alama ya tiki
  .
  • Wakati unarekodi ujumbe wa sauti, unaweza kubofya aikoni ya X ili ughairi.
Kwenye ujumbe wa sauti uliotumwa utaona:
 • Maikrofoni ya kijivu
  kwenye ujumbe wa sauti ambao mpokeaji wako hajaucheza.
 • Maikrofoni ya bluu
  kwenye ujumbe wa sauti ambao mpokeaji wako ameucheza.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La