Jinsi ya kutumia mbinu ya kufunga programu ya Android

Android
Kama hatua ya ziada ya faragha, unaweza kuwasha kipengele cha kufunga programu ya WhatsApp kwenye simu yako. Kikiwashwa, itabidi utumie alama ya kidole chako au uso ili kufungua programu. Bado unaweza kujibu simu ikiwa programu imefungwa.
Ili kutumia kipengele hiki, utahitaji kuweka bayometriki kama vile alama ya vidole au kuchanganua uso katika mipangilio ya simu yako.
Kuwasha mbinu ya kufunga programu
 1. Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Faragha.
 2. Telezesha hadi chini kisha uguse Kufunga programu.
 3. Washa Fungua kwa bayometriki.
 4. Gusa kitambuzi cha kidole au changanua uso wako ili uthibitishe.
 5. Unaweza kugusa ili uchague kiwango cha muda kabla ya uthibitisho wa alama ya kidole kutakiwa.
  • Washa Onyesha maudhui kwenye arifa ukitaka kuona muhtasari wa ujumbe wa maandishi ndani ya arifa za ujumbe mpya.
Kuzima mbinu ya kufunga programu
 1. Fungua WhatsApp > gusa Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Faragha.
 2. Telezesha hadi chini kisha uguse Kufunga programu.
 3. Zima Fungua kwa kutumia bayometriki.
Kumbuka:
 • Kipengele cha kufunga kwa alama ya kidole kinapatikana tu kwenye vifaa vya Android vilivyo na mfumo wa kutambua alama za kidole kwenye Android 6.0+ ambazo zinatumia API ya Google ya alama za vidole.
 • Uchanganuzi wa uso unapatikana tu kwenye vifaa vya Android vyenye kichanganuzi cha uso.
 • Kipengele hiki hakifanyi kazi kwenye Samsung Galaxy S5, Samsung Galaxy Note 4, au Samsung Galaxy Note 8.
 • Uthibitishaji kwa uso na alama za vidole hufanyika kikamilifu kwenye kifaa chako. Kwa makusudi, WhatsApp haiwezi kufikia taarifa za bayometriki zilizohifadhiwa na mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La