Matatizo ya arifa
Android
Kuhakikisha upokeaji wa jumbe za WhatsApp na arifa kwa mda muafaka, hakikisha simu yako imesanidiwa vizuri.
Hakikisha simu yako ina muunganisho wa intaneti
Unaweza kuangalia kwa kufungua kivinjari na kuenda kwenye tovuti. Ikiwa hii haifanyi kazi, tafadhali fuata hatua hizi za utatuaji wa muuganisho.
Ikiwa kuvinjari kunafanya kazi, lakini WhatsApp haifanyi, tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako wa simu ya mkononi na msimamizi wa mfumo na uhakikishe kwamba APN yako na kipanga njia zimesanidiwa kwa usahihi ili kuruhusu muunganisho usio wa wavuti na tundu. Unaweza pia kujaribu muunganisho tofauti. Ikiwa umeunganishwa na Wi-Fi, jaribu data ya simu au kinyume chake.
Hakikisha data ya nyuma haikuzuiwa
- Fungua kwenye simu yako Mipangilio programu > Programu > WhatsApp > Utumizi wa data.
- Hakikisha data ya nyuma haizuiwi.
- Rudia hatua za hapo juu kwa Huduma za Google.
Utatuaji ziada
- Anzisha upya simu yako au zima na washa.
- Anzisha mapendekezo ya programu yako kwa kuenda kwenye simu yako Mipangilio programu > Programu > Menyu ikoni > Anzisha mapendekezo ya programu.
- Zuia hali ya kuokoa nishati kuwezesha, kwa mfano kwa kuacha simu yako imeunganishwa na chanzo cha umeme.
- Jitoe WhatsApp Web kwa kwenda kwenye WhatsApp > Hiari zaidi> WhatsApp Web > Jitoe kwenye kompyuta zote.
- Washa Wi-Fi yako wakati wa muundo wa kulala kwa kwenda kwenye simu yako Mipangilio programu > Wi-Fi > Ikoni ya mipangilio > Washa Wi-Fi yako wakati wa muundo wa kulala > Kila mara.
- Ondoa viua jukumu vyovyote. Hizi zitazuia programu kutopokea jumbe wakati huitumii.
- Zindua programu ya Hangouts na ujiondoe kutoka kwa akaunti zako zote. Kisha zindua tena Hangouts na ingia tena.
Utatuaji maalum ziada wa OS
- Android 4.1 – 4.4
- Hakikisha kuwa data ya kusawazisha kiotomatiki imewashwa kwenye simu yako Mipangilio programu > Utumizi wa data > Menyu ikoni > data kusawazisha kiotomatiki.
- Hakikisha kuwa uboreshaji wa Wi-Fi umezimwa kwenye simu yako Mipangilioprogramu > Wi-Fi > Menyu ikoni > Juu > Uboreshaji wa Wi-Fi.
- Android 6.0+
- Hakikisha Usisumbue imezimwa au umeruhusu arifa za WhatsApp katika kwa kipaumbele kwenye simu yako Mipangilio programu > Sauti > Usisumbue.
- Hakikisha ruhusa zote za WhatsApp zinapewa kwenye simu yako Mipangilio programu > Programu > WhatsApp > Ruhusa.
Ikiwa hakuna hatua yoyote hapo juu itasaidia, inawezekana kwamba hupokei sasisho kutoka kwa huduma ya arifa ya Google.