Kuhusu historia ya ujumbe kwenye vifaa vilivyounganishwa

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mara tu baada ya kuunganisha kifaa, simu yako hutuma nakala ya hivi karibuni ya historia ya ujumbe wako uliofumbwa mwisho hadi mwisho kwenye kifaa chako kipya kilichounganishwa, ambapo ujumbe huo huhifadhiwa. Inaweza kuchukua dakika chache kwa historia ya ujumbe wako kuonekana kwenye vifaa vilivyounganishwa kutegemea idadi ya ujumbe ulio kwenye soga zako.
Kumbuka: Si ujumbe na soga zote husawazishwa kwenye vifaa vilivyounganishwa kutoka kwenye simu yako. WhatsApp Desktop husawazisha historia zaidi ya ujumbe kuliko WhatsApp Web. Ili uone au utafute historia yako kamili, angalia simu yako.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La