Jinsi ya kuweka akaunti ya WhatsApp Business kwenye Jalada la Instagram

Unapotumia programu ya WhatsApp Business, unaweza kuunganisha akaunti yako ya Instagram na akaunti yako ya WhatsApp Business.
Dokezo la Kibiashara: Kuunganisha akaunti yako ya kitaalamu ya Instagram na akaunti yako ya WhatsApp Business huwasha kitufe cha Bofya kwenye WhatsApp katika jalada lako la Instagram. Kitufe cha Bofya kwenye WhatsApp huwarahisishia wateja kuwasiliana na biashara yako na kuongeza mtagusano na wateja.
Ili kuunganisha akaunti hizi, lazima uwe na yafuatayo:
  • Akaunti ya Kitaalamu ya biashara yako kwenye Instagram.
  • Akaunti kwenye programu ya WhatsApp Business.
  • Matoleo ya hivi karibuni ya programu za vifaa vya mkononi.
Kuunganisha akaunti yako ya Instagram na programu ya WhatsApp Business
Unaweza kuunganisha akaunti zako za Instagram na WhatsApp Business kutoka kwenye programu ya WhatsApp Business.
  1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
  2. Kwenye Android, gusa Chaguo zaidi. Kwenye iPhone, gusa Mipangilio.
  3. Gusa Zana za biashara > Facebook na Instagram.
  4. Gusa Instagram > Endelea. Itafungua ukurasa wa kuingia kwenye Instagram.
  5. Weka maelezo ya kuingilia kwenye akaunti yako ya Instagram. Gusa Ingia. Unaweza pia kugusa Endelea na Facebook ili uingie kwa kutumia akaunti yako ya Facebook.
  6. Ikiwa tayari una Akaunti ya Kitaalamu kwenye Instagram, endelea katika hatua inayofuata. Ikiwa huna Akaunti ya Kitaalamu, utahitaji kusasisha aina ya akaunti yako.
    1. Gusa Inayofuata.
    2. Chagua Biashara au Muundaji. Kisha, gusa Inayofuata > Inayofuata > Inayofuata.
  7. Thibitisha maelezo ya akaunti yako. Gusa Ongeza > Rudi kwenye WhatsApp.
Mara unaporudi kwenye programu ya WhatsApp Business, utaona akaunti yako ya Kitaalamu ya Instagram iliyounganishwa ikionekana juu ya skrini ya Facebook na Instagram.
Kuondoa akaunti yako ya Instagram iliyounganishwa na programu ya WhatsApp Business
Ikiwa hutaki tena akaunti zako ziwe zimeunganishwa, unaweza kutenganisha akaunti yako ya Instagram na WhatsApp kutoka kwenye programu ya WhatsApp Business.
  1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
  2. Kwenye Android, gusa Chaguo zaidi. Kwenye iPhone, gusa Mipangilio.
  3. Gusa Zana za Biashara > Facebook na Instagram.
  4. Gusa akaunti yako iliyounganishwa ya Instagram > Ondoa WhatsApp > ONDOA.
Mara baada ya kuondoa akaunti yako, haitaonekana tena kwenye skrini ya Facebook na Instagram.
Kumbuka:
  • Si kila aina ya biashara kwenye Instagram inaweza kuwa kwenye programu ya WhatsApp Business. Ukiona ujumbe wa hitilafu unaosema “Aina ya biashara uliyo nayo kwenye Instagram haitumiki kwenye WhatsApp,” itabidi ubadili aina ya biashara uliyo nayo kwenye Instagram kuzingatia Sera ya Biashara ya WhatsApp ili uweze kuunganisha akaunti zako.
  • Ili kuunganisha akaunti zako, WhatsApp hushiriki taarifa ifuatayo na Facebook:
    • Maelezo kuhusu aina ya biashara uliyoweka kwenye WhatsApp hutumika kuweka aina yako ya biashara ya Kitaalamu kwenye Instagram ikiwa huna Akaunti ya Kitaalamu kwenye Instagram. Ikiwa tayari una Akaunti ya Kitaalamu kwenye Instagram, aina uliyo nayo kwenye WhatsApp Business haishirikiwi.
    • Nambari yako ya simu ya WhatsApp Business hutumiwa kuwawezesha wateja kukutumia ujumbe kwenye WhatsApp kutoka kwenye jalada lako la Instagram.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La