Kuhusu kupiga soga na biashara

Ni rahisi kutofautisha kati ya akaunti ya kibinafsi na akaunti ya biashara kwenye WhatsApp. Kwenye soga, gusa jina la unayewasiliana naye ili uone jalada lake. Ikiwa ni biashara, wasifu wake utajumuisha mojawapo ya lebo zifuatazo:
  • Akaunti ya biashara: Hii ndiyo hali chaguomsingi ya biashara inayofungua akaunti kwenye mojawapo ya bidhaa za WhatsApp Business.
    • Dokezo: Ikiwa jina la biashara linaonekana kwenye maelezo ya soga, hiyo inamaanisha kuwa WhatsApp imebaini chapa au biashara halali ndiyo inayomiliki akaunti hii. Jina la biashara hiyo linaonekana hata kama haujaongeza biashara hiyo kwenye kitabu chako cha anwani.
  • Akaunti rasmi ya biashara: WhatsApp imebaini kuwa chapa mashuhuri na halali ndiyo inayomiliki akaunti hii. "Akaunti rasmi ya biashara" ina beji ya tiki ya kijani kwenye jalada lake na karibu na kichwa katika orodha ya soga kati yako na biashara hiyo.
    • Dokezo: "Akaunti rasmi ya biashara" haionyeshi kuwa WhatsApp inaidhinisha biashara hii. Inamaanisha tu kwamba biashara inawakilisha mtu, chapa au shirika linalojulikana na lililotafutwa mara kwa mara kwenye intaneti.
Kwa nini ninaona ujumbe mpya wa mfumo kwenye soga zangu za WhatsApp?
Baadhi ya biashara unazowasiliana nazo kwa soga kwenye WhatsApp zinaweza kuchagua kutumia Facebook au kampuni nyingine kuzisaidia kudhibiti na kuhifadhi ujumbe wao.
Utaona ujumbe ufuatao, biashara inapochagua:
  • Kutumia mshirika: Utaona “Biashara hii hushirikiana na kampuni nyingine kushughulikia soga hii.”
  • Tumia Wingu la WhatsApp (Linalopangishwa na Meta): Utaona "Biashara hii hutumia huduma salama kutoka Meta ili kudhibiti soga hii."
Ikiwa biashara inadhibiti soga zake yenyewe, utaona: “Ujumbe na simu hufumbwa mwisho hadi mwisho. Hakuna yeyote nje ya soga hii, hata WhatsApp, anayeweza kusoma au kusikiliza.”
Ingawa Meta haitatumia ujumbe wako moja kwa moja kubaini matangazo utakayoona, biashara zitaweza kutumia soga zinazopokea kwa madhumuni yao ya kimauzo, ambayo huenda yakajumuisha kutangaza kwenye Meta.
Ikiwa hutaki kupokea ujumbe kutoka kwenye biashara, unaweza kuizuia moja kwa moja kwenye soga au uifute kutoka kwenye orodha yako ya anwani.
Salama na faragha wakati wote
Kila ujumbe wa WhatsApp hulindwa na itifaki ileile ya ufumbaji wa Ishara ambao hudumisha usalama wa ujumbe kabla haujatoka kwenye kifaa chako. Unapotuma ujumbe kwenda kwenye akaunti ya biashara ya WhatsApp, ujumbe wako hufikishwa kwa usalama kwenye sehemu iliyochaguliwa na biashara hiyo.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La