Â
Jinsi ya kutumia kipengele cha hali
Android
iPhone
KaiOS
Kipengele cha hali hukuwezesha kushiriki masasisho ya maandishi, picha, video na GIF yanayofumbwa mwisho hadi mwisho na ambayo hutoweka baada ya saa 24.
Kumbuka: Ili kutuma na kupokea masasisho ya hali kati yako na anwani zako, ni lazima nyote muwe mmehifadhi namba za kila mmoja wenu kwenye vitabu vya anwani vya simu zenu.
Kuunda na kutuma sasisho la hali
- Fungua WhatsApp > gusa Hali.
- Gusa:
- Kameraau Hali Yangu ili upige picha au urekodi video, GIF au uchague maudhui kwenye kiteuzi. Pia unaweza kuhariri au kuweka manukuu kwenye picha, video au GIF yako, kama inavyoelezwa kwenye makala haya. Kumbuka: WhatsApp hutumia video zenye muundo wa 3GP na mpeg4.
- Maandishiili utunge sasisho la hali kwa maandishi.
- T ili uchague fonti.
- Rangiili uchague rangi ya mandharinyuma.
- Sautikisha ushikilie ili urekodi sasisho la hali la sauti.
- Kamera
- Ili kuchagua hadhira kwa ajili ya hali, gusa hadhira yako chaguomsingi. Kisha, uchague anwani unazotaka zione hali yako > gusa Nimemaliza.
- Gusa Tuma.
Au unaweza kuunda na kutuma sasisho la hali la picha, video au GIF kutoka kwenye kichupo cha Soga kwa kugusa Kamera
.

Kumbuka: WhatsApp hutumia video zenye muundo wa 3GP na mpeg4.
Kuangalia au kujibu sasisho la hali
- Kuangalia sasisho la hali la anwani, gusa Hali, kisha sasisho la hali la anwani. Ili kujibu sasisho la hali la anwani, gusa Jibu.
Rasilimali