Â
Jinsi ya kutumia kipengele cha hali
Android
iPhone
KaiOS
Kipengele cha hali hukuwezesha kushiriki masasisho yanayofumbwa mwisho hadi mwisho kama maandishi, picha, video na GIF ambayo hutoweka baada ya saa 24.
Ili kutuma na kupokea masasisho ya hali kati yako na anwani zako, ni lazima nyote muwe mmehifadhi namba za kila mmoja wenu kwenye vitabu vya anwani vya simu zenu.
Kuunda na kutuma sasisho la hali
- Fungua WhatsApp > Hali.
- Gusa:
- Maandishiili utunge sasisho la hali kwa maandishi.
- Emoji ili uweke emoji au GIf.
- T ili uchague fonti.
- Rangiili uchague rangi ya mandharinyuma.
- Sautikisha ushikilie ili urekodi sasisho la hali la sauti.
- Kameraau Hali yangu ili upige picha, urekodi video, GIF au uchague maudhui kutoka kwenye kiteuzi. Pia unaweza kuhariri au kuweka manukuu kwenye picha, video au GIF yako, kama inavyoelezwa kwenye makala haya. Kumbuka: WhatsApp hutumia video zenye muundo wa 3GP na mpeg4.
- Chagua hadhira kwa ajili ya hali kwa kugusa hadhira yako chaguomsingi. Kisha, uchague anwani unazotaka zione hali yako kisha uguse Nimemaliza.
- Gusa Tuma.
Au unaweza kuunda na kutuma hali ya picha, video au GIF kutoka kwenye kichupo cha Soga kwa kugusa Kamera
.

Kuangalia au kujibu sasisho la hali
Unaweza kuangalia sasisho la hali la anwani uliyohifadhi kwa kwenda kwenye kichupo cha Hali na kugusa sasisho lake la hali.
Ili kujibu sasisho la hali la anwani, gusa Jibu wakati unaliangalia.
Rasilimali