WhatsApp Business ni nini?

WhatsApp Business ni programu unayoweza kupakua bila malipo kwenye Android na iPhone na iliundwa kwa kuwazingatia wamiliki wa biashara ndogo. WhatsApp Business hurahisisha kutangamana na wateja kwa kutoa zana za kufanya kupanga na kujibu ujumbe kuwe haraka na wa kiotomatiki. Pia imenuiwa kuwa na kufanya kazi kama WhatsApp Messenger. Unaweza kuitumia kufanya kila kitu ulichozoea kufanya, kutuma ujumbe na hata kutuma picha.
Baadhi ya vipengele ambavyo kwa sasa vipo katika programu ni pamoja na:
  • Jalada la biashara ili kuorodhesha taarifa muhimu, kama vile anwani ya kampuni, anwani ya barua pepe na tovuti.
  • Lebo ili kupanga na kupata soga na ujumbe wako kwa urahisi.
  • Zana za utumaji ujumbe ili kuwajibu wateja kwa haraka.
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuipakua kutoka kwenye Duka la Google Play na App Store.
Ikiwa huna biashara, hakuna haja ya kupakua programu hii tofauti. Unaweza kuendelea kutumia akaunti yako ya WhatsApp Messenger bure ili kuzungumza na marafiki, familia na biashara.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La