Jinsi ya kuripoti orodha au biashara

Ikiwa unafikiria biashara inakiuka Sera ya Biashara yetu, unaweza kuiripoti.
Ripoti bidhaa au huduma
 1. Fungua soga na biashara.
 2. Gusa jina la biashara kuona jalada lao la WhatsApp Business.
 3. Gusa ONA YOTE karibu na Orodha.
 4. Gusa bidhaa au huduma kutazama Maelezo.
 5. Gusa Hiari zaidi
  > Ripoti.
 6. Una hiari mbili:
  • Kuripoti bidhaa au huduma tu, gusa RIPOTI.
  • Kutoa maelezo zaidi, gusa TUELEZE ZAIDI. Kisha, chagua hiari na gusa WASILISHA.
Ripoti biashara
 1. Nenda kwenye jalada la WhatsApp Business.
 2. Gusa Ripoti biashara.
 3. Una hiari mbili:
  • Kuzuia na kuripoti biashara, gusa kisanduku tiki karibu na Zuia mwasiliani na futa jumbe za soga hizi. Kisha, gusa RIPOTI.
  • Kuripoti biashara tu, gusa RIPOTI.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La