Jinsi ya kutuma maudhui

Kushiriki maudhui, hati, mahali au anwani
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Gusa Ambatisha
  . Kisha, gusa:
  • Hati ili kuchagua hati kutoka kwa simu yako.
  • Kamera ili kupiga picha kwa kamera yako.
  • Matunzio ili kuchagua picha au video iliyopo kutoka kwa simu yako. Gusa na shikilia ili kuchagua picha nyingi.
  • Sauti ili kutuma sauti iliyopo kutoka kwa simu yako.
  • Mahali ili kutuma mahali pako au mahali pa karibu.
  • Anwani ili kutuma taarifa za mtu aliyehifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako kupitia WhatsApp.
 3. Unaweza pia kuongeza manukuu kwenye picha na video. Telezesha kidole kati ya picha ili kuongeza muktasari kwa kila moja.
 4. Gusa Tuma
  .
Kumbuka: Ukubwa wa juu unaoruhusiwa wa hati ni GB 2. Ili kutuma hati ndani ya WhatsApp, hati hizo lazima zihifadhiwe kwenye simu yako. Vinginevyo, WhatsApp itaonekana kama chaguo katika menyu ya kushiriki ya programu zinazoshughulikia hati. Unapopakua hati, itahifadhiwa kiotomatiki katika folda yako ya Hati za WhatsApp: WhatsApp/Media/WhatsApp Documents, ambayo inaweza kufikiwa kwa programu ya kufungua faili.
Sambaza maudhui, hati, mahali au anwani
 1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
 2. Gusa na ushikilie aina ya ujumbe unaotaka kusambaza. Unaweza kuchagua ujumbe kadhaa.
 3. Gusa Sambaza
  .
 4. Chagua soga unayotaka kuisambazia ujumbe.
 5. Gusa Tuma
  .
Unaposambaza maudhui, hati, maeneo au anwani, huhitaji kuzipakia tena. Ujumbe wowote uliosambazwa ambao awali haukutumwa nawe utaonyesha lebo ya "Imesambazwa".
Kumbuka: Manukuu hayatasambazwa pamoja na maudhui. Hautaweza kusambaza ujumbe kwa orodha za matangazo.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La