Jinsi ya kuongeza nambari ya simu ya kimataifa

  1. Fungua kitabu cha anwani cha simu yako.
  2. Unapoongeza nambari ya simu ya mwasiliani, anza kwa kuongeza alama ya jumlisha (+).
  3. Ingiza msimbo wa nchi, ukifuatiwa na nambari kamili ya simu.
    • Dondoo: Msimbo wa nchi ni kiambishi cha nambari ambacho kinahitajika kuingizwa kabla ya nambari kamili ya simu ya kitaifa ili kupiga simu kwa nchi nyingine. Unaweza kutafuta mtandaoni ili kupata msimbo wa nchi unayohitaji.
Kwa mfano, ikiwa mwasiliani aliyepo Marekani (msimbo wa nchi “1”) ana msimbo wa eneo “408” na nambari ya simu "XXX-XXXX", utaingiza +1 408 XXX XXXX.
Dondoo:
  • Hakikisha kuondoa 0 zozote zinazoongoza au misimbo maalum ya kupiga simu.
  • Ikiwa una maana ya kuongeza nambari ya simu ya eneo (katika nchi) kwa kitabu chako cha anwani ya simu, ingiza nambari kama unavyompigia simu mwasiliani wako.
  • Nambari zote za simu nchini Ajentina (msimbo wa nchi "54") zinapaswa kuwa na "9" kati ya msimbo wa nchi na msimbo wa eneo. Kiambishi "15" lazima kiondolewe ili nambari ya mwisho iwe na tarakimu 13 kwa jumla: +54 9 XXX XXX XXXX
  • Nambari za simu nchini Meksiko (msimbo wa nchi "52") zinahitajika kuwa na "1" baada ya "+52", hata kama ni nambari za Nextel.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La