Jinsi ya kutumia vibandiko

Android
iPhone

Kupakua na kutumia vibandiko:
  1. Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
  2. Kuongeza vifurushi vya vibandiko, gusa Vibandiko
    > Ongeza
    .
  3. Gusa Pakua
    karibu na kifurushi cha vibandiko unachotaka kupakua. Ukiulizwa, gusa Pakua • {ukubwa wa faili}.
    • Alama ya tiki
      itatokea mara tu upakuaji utakapokamilika.
  4. Telezesha chini kwenye ibukizi la Vibandiko.
  5. Tafuta na uguse kibandiko unachotaka kutuma.
Baada ya kugusa kibandiko, kitatumwa kiotomatiki.
Hiari zaidi:
  • Gusa Hivi karibuni
    ili uone vibandiko ulivyotumia hivi karibuni
  • Gusa Vipendwa
    ili uone vibandiko unavyopendelea.
    • Kufanya kibandiko kiwe kwenye vipendwa, gusa kibandiko juujuu katika soga ya binafsi au ya kikundi > Ongeza kwenye Vipendwa. Au, gusa Vibandiko
      . Gusa na ushikilie kibandiko, kisha uguse Ongeza kwenye Vipendwa.
    • Kuondoa kibandiko kwenye vipendwa, gusa kibandiko juujuu kwenye soga ya binafsi au ya kikundi > Ondoa kwenye Vipendwa. Au, gusa Vibandiko
      > Vipendwa
      . Gusa na ushikilie kibandiko, kisha uguse Ondoa kwenye Vipendwa.
  • Gusa Tafuta
    ili utafuta vibandiko mahususi ambavyo umepakua. Unaweza kutafuta vibandiko kwa kutumia maandishi au emoji.
    • Kumbuka: Vibandiko unavyopakua nje ya WhatsApp huenda visiweze kutafutika ikiwa muundaji wa kibandiko hakufuata miongozo ya WhatsApp ya kuwekea vibandiko lebo.
    • Utafutaji wa vibandiko hufanyika nje ya mtandao kabisa. WhatsApp haikusanyi taarifa kuhusu utumiaji wako wa utafutaji wa vibandiko au maneno ya msingi unayotumia wakati wa kutafuta vibandiko.
  • Vibandiko vimewekwa kwenye makundi kwa kutegemea emoji zinazoonekana kwenye aikoni. Gusa kisanduku cha moyo
    ili uone makundi ya vibandiko.
  • Ili uone vifurushi vya vibandiko ambavyo umepakua, gusaOngeza
    > Vibandiko Vyangu.
    • Ukitaka kufuta kifurushi fulani cha kibandiko, gusa kifurushi husika cha vibandiko > Futa > Futa.
    • Kubadilisha mpangilio wa vifurushi vyako vya vibandiko, gusa Hariri. Kisha, gusa na ushikilie Panga upya
      karibu na kifurushi cha vibandiko halafu kiburute juu au chini.
  • Ili usasishe vifurushi vya vibandiko, gusa Ongeza
    pindi ukiona kitone cha buluu. Kwenye kichupo cha Vibandiko Vyote, gusa SASISHA iliyo karibu na vifurushi vya vibandiko vinavyohitaji kusasishwa. Ukiulizwa, gusa Sasisha • {ukubwa wa faili}.
    • Alama ya tiki
      itatokea mara tu usasishaji utakapokamilika.
Vibandiko vinapatikana kwenye matoleo ya hivi karibuni ya WhatsApp. Kama huoni vibandiko, tafadhali hakikisha unasasisha na kupata toleo jipya la WhatsApp.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La