Â
Jinsi ya kutumia vibandiko
Android
iPhone
Kupakua na kutumia vibandiko
- Fungua soga ya binafsi au ya kikundi.
- Kuongeza vifurushi vya vibandiko, gusa Emoji> Vibandiko> Ongeza.
- Gusa Pakuakaribu na kifurushi cha vibandiko unachotaka kupakua. Ukiulizwa, gusa PAKUA • {ukubwa wa faili}.
- Alama ya tiki ya kijani itatokea mara tu upakuaji utakapokamilika.
- Alama ya tiki ya kijani
- Gusa Rudi.
- Tafuta na uguse kibandiko unachotaka kutuma.
Baada ya kugusa kibandiko, kitatumwa kiotomatiki.
Hiari zaidi:
- Gusa Karibuniili uone vibandiko ulivyotumia hivi karibuni.
- Gusa Vipendwaili uone vibandiko unavyopendelea.
- Ili uongeze kibandiko kwenye vipendwa, gusa Emoji> Vibandiko. Gusa na ushikilie kibandiko, kisha gusa ONGEZA. Au, gusa kibandiko ukiwa kwenye dirisha la soga kati yako na mtu binafsi au kikundi ONGEZA KWENYE VIPENDWA.
- Ili uondoe kibandiko kwenye vipendwa, gusa Emoji> Vibandiko> Vipendwa. Gusa na ushikilie kibandiko, kisha gusa ONDOA. Au, gusa kibandiko ukiwa kwenye dirisha la soga kati yako na mtu binafsi au kikundi ONDOA KWENYE VIPENDWA.
- Ili uongeze kibandiko kwenye vipendwa, gusa Emoji
- Vibandiko huwekwa katika makundi kwa kutegemea emoji zinazoonekana kwenye aikoni. Gusa kisanduku cha moyo ili uone makundi ya vibandiko.
- Gusa Ongezaili upate machaguo zaidi ya vibandiko. Sogeza mpaka mwisho wa kichupo cha VIBANDIKO VYOTE halafu uguse PATA VIBANDIKO ZAIDI. Kufanya hivyo kutakupeleka kwenye Duka la Google Play, ambapo utaweza kupakua programu za vibandiko.
- Gusa Tafutaili utafute vibandiko mahususi ulivyoovipakua. Unaweza kutafuta vibandiko kwa kutumia maandishi au emoji.
- Kumbuka: Vibandiko unavyopakua nje ya WhatsApp huenda visiweze kutafutika ikiwa muundaji wa kibandiko hakufuata miongozo ya WhatsApp ya kuwekea vibandiko lebo.
- Utafutaji wa vibandiko hufanyika nje ya mtandao kabisa. WhatsApp haikusanyi taarifa kuhusu utumiaji wako wa utafutaji wa vibandiko au maneno ya msingi unayotumia wakati wa kutafuta vibandiko.
- Ili uone vifurushi vya vibandiko ambavyo umepakua, gusa Ongeza> VIBANDIKO VYANGU.
- Ikiwa unataka kufuta kibandiko mahususi, gusa Futa> FUTA.
- Ili kupanga vibandiko vyako upya, gusa na uburute Panga upyakaribu na furushi la kibandiko.
- Ili usasishe vifurushi vya vibandiko, gusa Ongezapindi kitone cha kijani kikitokea. Kwenye kichupo cha VIBANDIKO VYOTE, gusa SASISHA karibu na vifurushi vya vibandiko vinavyohitaji kusasishwa. Ukiulizwa, gusa SASISHA • {ukubwa wa faili}.
- Alama ya tiki ya kijani itatokea mara tu sashisho litakapokamilika.
- Alama ya tiki ya kijani
Vibandiko vinapatikana kwenye matoleo ya hivi karibuni ya WhatsApp. Kama huoni vibandiko, hakikisha unasasisha ili upate toleo jipya zaidi la WhatsApp kwenye duka la programu la simu yako.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kuunda vibandiko