Jinsi ya kudhibiti wasimamizi wa kikundi

Android
iOS
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Mac
Kikundi kinaweza kuwa na idadi yoyote ya wasimamizi na msimamizi yeyote anaweza kumfanya mshiriki kuwa msimamizi. Mtu ambaye ameunda kikundi hawezi kuondolewa na atabaki kuwa msimamizi isipokuwa akiondoka kwenye kikundi.
Kumbuka: WhatsApp haiwezi kuingilia utendaji wa usimamizi wa kikundi. Kwa mfano, hatuwezi kumfanya mtu kuwa msimamizi.
Kumfanya mshiriki kuwa msimamizi
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye jina.
  • Au bofya
   more options
   au
   menu
   katika kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 2. Wekelea kiashiria kwenye anwani ya mshiriki ambaye ungependa kumfanya kuwa msimamizi, kisha ubofye
  menu
  .
 3. Bofya Mfanye kuwa msimamizi wa kikundi > Mfanye kuwa msimamizi wa kikundi.
Kuwafanya washiriki wengi kuwa wasimamizi kwa wakati mmoja
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye jina.
  • Au bofya
   more options
   au
   menu
   iliyo katika kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 2. Bofya Mipangilio ya Kikundi > Hariri wasimamizi wa kikundi.
 3. Chagua washiriki ambao ungependa kuwafanya kuwa wasimamizi.
 4. Bofya alama hakikishi ya kijani unapomaliza.
Kumwondoa msimamizi kuwa msimamizi
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye jina.
  • Au bofya
   more options
   au
   menu
   katika kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 2. Wekelea kiashiria kwenye msimamizi ambaye ungependa kumwondoa kuwa msimamizi, kisha ubofye
  menu
  > Mwondoe kuwa msimamizi.
Kuwaondoa wasimamizi wengi kwa wakati mmoja
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubofye jina.
  • Au bofya
   more options
   au
   menu
   iliyo katika kona ya juu > Maelezo ya kikundi.
 2. Bofya Mipangilio ya Kikundi > Hariri wasimamizi wa kikundi.
 3. Ondoa tiki kwenye wasimamizi unaotaka kuwaondoa kuwa wasimamizi.
 4. Bofya alama hakikishi ya kijani unapomaliza.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La