Jinsi ya kudhibiti wasimamizi wa kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Msimamizi yeyote kwenye kikundi anaweza kumfanya mshiriki awe msimamizi. Kikundi kinaweza kuwa na idadi yoyote ya wasimamizi. Mtu ambaye ameunda kikundi hawezi kuondolewa na atabaki kuwa msimamizi isipokuwa akiondoka kwenye kikundi.
Kumfanya mshiriki kuwa msimamizi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubonyeze Chaguo > Maelezo ya kikundi.
    • Au, chagua kikundi kwenye orodha ya Soga zako. Kisha, ubonyeze Chaguo > Maelezo ya kikundi.
  2. Chagua mshiriki unayetaka kumfanya kuwa msimamizi.
  3. Bonyeza Chaguo > Mfanye kuwa msimamizi wa kikundi.
Kumwondoa msimamizi kuwa msimamizi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha ubonyeze Chaguo > Maelezo ya kikundi.
    • Au, chagua kikundi kwenye orodha ya Soga zako. Kisha, ubonyeze Chaguo > Maelezo ya kikundi.
  2. Chagua msimamizi unayetaka kumwondoa kuwa msimamizi.
  3. Bonyeza Chaguo > Mwondoe kuwa msimamizi.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La