Jinsi ya kusimamia wasimamizi wa kikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Msimamizi yeyote katika kikundi anaweza kumfanya mshiriki awe msimamizi. Kikundi kinaweza kuwa na idadi isiyo na kikomo ya wasimamizi. Mtu aliyeanzisha kikundi hawezi kuondolewa na atabaki kuwa msimamizi isipokuwa aondoke kwenye kikundi.
Kumfanya mshiriki kuwa msimamizi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
    • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha, gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
  2. Gusa mshiriki unayetaka kumfanya msimamizi.
  3. Gusa Mfanye msimamizi wa kikundi.
Kuwafanya washiriki wengi wasimamizi kwa wakati mmoja
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
    • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha, gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
  2. Gusa Mipangilio ya Kikundi > Badili Wasimamizi wa Kikundi.
  3. Chagua washiriki unaotaka kuwafanya wasimamizi.
  4. Gusa Nimemaliza.
Kuondoa msimamizi
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
    • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha, gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
  2. Gusa msimamizi unayetaka kumwondoa.
  3. Gusa Mwondoe kuwa msimamizi.
Kuwaondoa wasimamizi wengi kwa wakati mmoja
  1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
    • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha, gusa Zaidi > Maelezo ya kikundi.
  2. Gusa Mipangilio ya Kikundi > Badili Wasimamizi wa Kikundi.
  3. Ondoa tiki kwenye wasimamizi unaotaka kuwaondoa.
  4. Gusa Nimemaliza.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La