Jinsi ya kuweka au kuondoa akaunti yako ya WhatsApp kwenye Portal

Kuweka akaunti yako
Kumbuka: Ukiamua kuweka akaunti yako ya WhatsApp, waasiliani wako hawashirikiwi na Facebook, lakini watahifadhiwa kwenye kifaa cha Portal.
  1. Kwenye Portal yako, gusa au chagua Mipangilio > Akaunti > jina lako > Unganisha WhatsApp. Utaona msimbo ambao utahitaji kuutumia ili uingie kwenye Facebook.
  2. Fungua facebook.com/device kwenye kivinjari cha simu au kompyuta yako. Ikiwa unatumia:
    • Simu: Gusa WEKA MSIMBO. Weka msimbo, halafu gusa ENDELEA > Thibitisha.
    • Kompyuta: Weka msimbo, halafu bofya Endelea > Thibitisha.
  3. Kwenye Portal yako, chagua Kwa kuchagua, unakubali kupokea ujumbe kutoka kwenye Portal katika WhatsApp.
  4. Gusa au chagua Endelea > Inayofuata.
  5. Fungua WhatsApp kwenye simu yako.
    • Android: Gusa Chaguo zaidi
      > Vifaa Vilivyounganishwa > UNGANISHA KIFAA. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ikiwa kifaa chako kina uthibitishaji wa bayometriki. Ikiwa hujawasha uthibitishaji wa bayometriki, utaombwa uweke PIN ambayo huwa unatumia kufungua simu yako.
    • iPhone: Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp > gusa Vifaa Vilivyounganishwa > Unganisha Kifaa > SAWA. Kwenye iOS 14 na matoleo ya baadaye, tumia Touch ID au Face ID kufungua. Ikiwa hujawasha uthibitishaji wa bayometriki, utaombwa uweke PIN ambayo huwa unatumia kufungua simu yako.
  6. Tumia simu yako kuchanganua msimbo wa QR ulio kwenye Portal yako.
  7. Kwenye Portal yako, gusa au chagua Nimemaliza.
Kumbuka: Uthibitishaji hushughulikiwa na mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako kwa kutumia alama za bayometriki zilizohifadhiwa humo. WhatsApp haiwezi kufikia taarifa za bayometriki zilizohifadhiwa kwenye mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako.
Kuondoa akaunti yako
  1. Kwenye Portal yako, gusa au chagua Mipangilio > Akaunti > jina lako > WhatsApp > Ondoa Akaunti.
  2. Fungua WhatsApp kwenye simu au WhatsApp Web au WhatsApp Desktop kwenye kompyuta yako.
  3. Fungua soga husika iliyo na "Portal kutoka Facebook" ili uone msimbo wa uthibitishaji uliotumwa.
  4. Kwenye Portal yako, weka msimbo wa uthibitishaji, halafu gusa au chagua Nimemaliza > Ondoa.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La