Jinsi ya kuweka au kuondoa akaunti yako ya WhatsApp kwenye Portal

Kuweka akaunti yako
Kumbuka: Ikiwa utaamua kuweka akaunti yako ya WhatsApp, anwani zako hazitashirikiwa na Facebook, lakini zitahifadhiwa kwenye kifaa cha Portal.
 1. Kwenye Portal yako, gusa au uchague Programu > Mipangilio > Majalada.
 2. Gusa au uchague jina lako, kisha uweke msimbo wako wa siri.
 3. Gusa au uchague Unganisha WhatsApp. Utaona msimbo ambao utahitaji kuutumia ili uingie kwenye akaunti ya Facebook.
 4. Fungua facebook.com/device kwenye kivinjari cha simu au kompyuta yako. Ikiwa unatumia:
  • Simu: Gusa WEKA MSIMBO. Weka msimbo, kisha uguse ENDELEA > Thibitisha.
  • Kompyuta: Weka msimbo, kisha ubofye Endelea > Thibitisha.
 5. Kwenye Portal yako, gusa au uchague kisanduku cha kuteua Kwa kuchagua, unakubali kupokea ujumbe unaotoka kwenye Portal katika WhatsApp.
 6. Gusa au uchague Endelea > Inayofuata.
 7. Fungua WhatsApp kwenye simu yako.
  • Android: Gusa
   more options
   > Vifaa vilivyounganishwa > Unganisha kifaa. Fuata maelekezo kwenye skrini ikiwa umewasha kipengele cha kuthibitisha kwa njia ya bayometriki kwenye kifaa chako. Ikiwa hujawasha kipengele cha uthibitishaji kwa njia ya bayometriki, utaombwa uweke PIN ambayo huwa unatumia kufungua simu yako.
  • iPhone: Nenda kwenye Mipangilio ya WhatsApp > gusa Vifaa Vilivyounganishwa > Unganisha Kifaa > SAWA. Kwenye toleo la iOS 14 na matoleo mapya, tumia Touch ID au Face ID kufungua. Ikiwa hujawasha kipengele cha uthibitishaji kwa njia ya bayometriki, utaombwa uweke PIN ambayo huwa unatumia kufungua simu yako.
 8. Tumia simu yako kuchanganua msimbo wa QR utakaoonyeshwa kwenye Portal yako.
 9. Kwenye Portal yako, gusa au uchague Nimemaliza.
Kumbuka: Uthibitishaji hushughulikiwa na mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako kwa kutumia alama za bayometriki zilizohifadhiwa humo. WhatsApp haiwezi kufikia maelezo ya bayometriki yanayohifadhiwa kwenye mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako.
Kuondoa akaunti yako ya WhatsApp kwenye Portal
 1. Kwenye Portal yako, gusa au uchague Programu > Mipangilio > Majalada.
 2. Gusa au uchague jina lako, kisha uweke msimbo wako wa siri.
 3. Gusa au uchague WhatsApp > Ondoa kwenye Portal > Ondoa.
 4. Fungua WhatsApp kwenye simu yako au WhatsApp Web au WhatsApp Desktop kwenye kompyuta yako.
 5. Fungua soga ya mtu binafsi kwenye Portal kutoka Facebook ili uangalie msimbo wa uthibitishaji uliotumwa.
 6. Kwenye Portal yako, weka msimbo wa uthibitishaji, kisha uguse au uchague kisanduku cha kuteua au Nimemaliza.
Rasilimali zinazohusiana
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La