Â
Jinsi ya kurejesha historia ya soga zako
Android
iPhone
Rejesha historia yako ya soga kutoka kwa chelezo ya iCloud
- Thibitisha kuwa kuna chelezo ya iCloud kwenye WhatsApp > Mipangilio > Soga > Chelezo ya Soga.
- Ikiwa unaweza kuona ni lini chelezo la mwisho lilifanywa, futa na sakinisha upya WhatsApp.
- Baada ya kuthibitisha namba yako ya simu, fuata maagizo ili kurejesha historia yako ya soga.
Dondoo:
- Lazima uingie ndani na ID ya Apple unayotumia kuingia kwenye iCloud na lazima iCloud Drive iwashwe.
- Ni lazima kuwe na nafasi ya kutosha kwa iCloud na iPhone. Unahitaji angalau mara 2.05 ya nafasi huru kwenye akaunti yako ya iCloud na kwenye simu yako kuliko nafasi kamili ya chelezo yako.
- Namba ya simu iliyotumiwa kwa kucheleza na kurejesha lazima ziwe sawa. Huwezi kurejesha historia ya soga kutoka kwa akaunti nyingine ya WhatsApp.
- Kwa kuwa chelezo zina husishwa na nambari ya simu, inawezekana kuwa na chelezo kadhaa kwa akaunti ya WhatsApp kwenye akaunti hiyohiyo ya iCloud.
Rasilimali zinazohusiana:
- Jinsi ya kucheleza kwenye iCloud
- Siwezi kuunda au kurejesha chelezo la iCloud