Jinsi ya kurejesha historia ya soga zako

Android
iPhone
Ili kuhakikisha kuwa soga zako zimenakiliwa kabla ya kuzirejesha kwenye kifaa kipya cha Android:
 1. Fungua WhatsApp > Chaguo zaidi
  > Mipangilio > Soga > Nakala ya soga.
 2. Chagua akaunti ya Google ambayo unataka kutumia kuhifadhi nakala ya soga zako. Unaweza pia kuunda nakala kwenye kifaa chako.
 3. Gusa HIFADHI NAKALA.
 4. Baada ya kuhifadhi nakala, unaweza kuondoa WhatsApp kutoka kwenye kifaa chako na kuisakinisha kwenye kifaa chako kipya cha Android.
Kurejesha kutoka kwenye nakala rudufu ya Hifadhi ya Google
Ili kudumisha nakala ya historia yako ya soga kwenye Hifadhi ya Google, unaweza kuwasha kipengele cha kuhifadhi nakala kiotomatiki kwa soga zako na uchague marudio yake iwe kila siku, kila juma au kila mwezi. Ili uweze kurejesha nakala rudufu iliyo kwenye Hifadhi ya Google, unahitaji kutumia nambari ya simu na akaunti ile ile ya Google uliyotumia kuunda nakala rudufu.
Kurejesha nakala zako:
 1. Hakikisha kuwa kifaa chako kipya cha Android kimeunganishwa kwenye Akaunti ya Google ambapo nakala yako imehifadhiwa
 2. Sakinisha na ufungue WhatsApp, kisha uthibitishe nambari yako.
 3. Gusa REJESHA unapoulizwa kurejeshe soga zako na maudhui kutoka kwenye Hifadhi ya Google.
 4. Baada ya mchakato wa kurejesha kukamilika, gusa INAYOFUATA. Soga zako zitaonyeshwa mara uanzishaji ukikamilika.
 5. WhatsApp itaendelea kurejesha faili zako za maudhui baada ya kurejesha soga zako.
Kama unasakinisha WhatsApp bila nakala zozote za awali kutoka kwenye Hifadhi ya Google, WhatsApp itarejesha kiotomatiki nakala kutoka kwenye hifadhi ya kifaa chako.
Kurejesha kutoka kwenye nakala ya ndani
Ikiwa unataka kutumia nakala rudufu iliyo kwenye kifaa, utahitaji kuhamishia faili kwenye simu kwa kutumia kompyuta, uhamishaji wa faili au kadi ya SD.
Kurejesha nakala zako:
 1. Pakua programu ya kudhibiti faili.
 2. Kwenye programu ya kudhibiti faili, elekea kwenye hifadhi yako ya ndani au sdcard > WhatsApp > Hifadhidata. Ikiwa data yako haijahifadhiwa kwenye kadi ya SD, unaweza kuona "hafidhi ya ndani" au "hifadhi kuu" badala yake. Nakili faili ya hivi karibuni ya nakala kwenye folda ya Hifadhidata ya kifaa chako kipya.
 3. Sakinisha na ufungue WhatsApp, kisha uthibitishe nambari yako.
 4. Gusa REJESHA unapoulizwa kurejeshe soga zako na maudhui kutoka kwenye hifadhi ya ndani.
Kumbuka:
 • Simu yako inahifadhi angalau faili za kiasi cha siku saba za nakala rudufu ya ndani ya kifaa.
 • Nakala rudufu za ndani ya kifaa huundwa kiotomatiki kila siku saa 8 usiku na kuhifadhiwa kama faili kwenye simu yako.
 • Ikiwa data yako haijahifadhiwa kwenye folda ya /sdcard/WhatsApp/, unaweza kuona folda za "hifadhi ya ndani" au "hifadhi kuu".
Kurejesha nakala rudufu ya ndani ambayo si ya hivi karibuni
Ikiwa unataka kurejesha nakala rudufu ya ndani ambayo si ya hivi karibuni, utahitaji kufanya yafuatayo:
 1. Pakua programu ya kudhibiti faili.
 2. Kwenye programu ya kudhibiti faili, elekea kwenye hifadhi yako ya ndani au sdcard > WhatsApp > Hifadhidata. Ikiwa data yako haijahifadhiwa kwenye kadi ya SD, unaweza kuona "hafidhi ya ndani" au "hifadhi kuu" badala ya sdcard.
 3. Lipatie jina jipya nakala rudufu unayotaka kurejesha kutoka msgstore-YYYY-MM-DD.1.db.crypt12 hadi msgstore.db.crypt12. Inawezekana kwamba nakala yako rudufu ya awali inaweza kuwa inatumia itifaki ya awali, kama vile crypt9 au crypt10. Usibadilishe nambari ya mwisho ya crypt.
 4. Ondoa na usakinishe tena WhatsApp.
 5. Gusa REJESHA unapoulizwa.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La