Jinsi ya kushiriki bidhaa au huduma na wateja

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Android
iPhone
Unaweza kushiriki bidhaa na huduma zako na wateja wapya na waliopo kwa kushiriki katalogi yako.
Shiriki katalogi yako kwenye soga ya kibinafsi au soga ya kikundi
 1. Fungua soga kwenye programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa aikoni ya kiambatisho karibu na uga wa maandishi.
 3. Kisha, gusa Katalogi.
 4. Gusa Tuma vitu vyote hapo juu.
Shiriki bidhaa au huduma kwenye soga ya kibinafsi au soga ya kikundi
 1. Fungua soga kwenye programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa aikoni ya kiambatisho karibu na uga wa maandishi.
 3. Kisha, gusa Katalogi.
 4. Teua bidhaa au huduma unayo taka shiriki.
 5. Gusa Tuma.
Shiriki katalogi yote kupitia kwa Kisimamizi cha Katalogi
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
 2. Mara unapokuwa kwenye Kisimamizi cha Katalogi, gusa aikoni ya kiungo kilichopo juu upande wa kulia.
 3. Kisha unaweza kushiriki katalogi nzima na waasiliani wako au wanunuzi tarajiwa popote kwa kuchagua hiari yoyote:
  • Tuma kiungo kupitia WhatsApp Business: kushiriki kiungo cha katalogi na wengine kwa WhatsApp
  • Nakili Kiungo: kunakili kiungo
  • Shiriki Kiungo: kushiriki katalogi kupitia barua pepe au programu zingine za utumaji ujumbe.
Shiriki bidhaa au huduma binafsi kupitia Kisimamizi cha Katalogi
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business > Mipangilio > Zana za Biashara > Katalogi.
 2. Kutoka kwa Kisimamizi cha Katalogi, chagua vitu unavyotaka kushiriki. Kisha, gusa aikoni ya kiungo iliyopo juu upande wa kulia.
 3. Unaweza kushiriki kitu maalumu kwenye katalogi yako na waasiliani wako au wanunuzi tarajiwa popote pale kwa kuchagua hiari yoyote:
  • Tuma kiungo kupitia WhatsApp Business: kushiriki viungo vya vitu vilivyoteuliwa na wengine kupitia WhatsApp
  • Nakili Kiungo: kunakili kiungo
  • Shiriki Kiungo: kushiriki kitu kilichochaguliwa kwa njia ya barua pepe au vituo vya jamii.
Katalogi na viungo vya vitu haviwezi kubinafsishwa kabla ya kushirikishwa kwani vinatolewa kiotomatiki.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La