Jinsi ya kufanya mabadiliko kwenye vikundi

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Kwa chaguomsingi, mshiriki yeyote wa kikundi anaweza kubadili mada, aikoni, maelezo au kutuma ujumbe. Hata hivyo, msimamizi wa kikundi anaweza kubadilisha mipangilio ya kikundi ili kuruhusu wasimamizi pekee kuhariri maelezo ya kikundi.
Kubadilisha maelezo ya kikundi
Kubadili mada ya kikundi
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha gusa Zaidi
   > Maelezo ya Kikundi.
 2. Gusa mada ya kikundi.
 3. Weka mada mpya, kisha gusa Hifadhi.
  • Ukomo wa mada ni herufi 25.
Kubadilisha aikoni ya kikundi
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha gusa Zaidi
   > Maelezo ya Kikundi.
 2. Gusa Kamera
  .
 3. Chagua Badilisha Aikoni, Piga Picha, Chagua Picha, Emoji na Vibandiko, au Tafuta Mtandaoni ili uweke picha mpya.
Kubadilisha maelezo ya kikundi
 1. Fungua soga husika ya kikundi cha WhatsApp, kisha gusa mada ya kikundi.
  • Au, telezesha kikundi upande wa kushoto kwenye kichupo cha Soga. Kisha gusa Zaidi
   > Maelezo ya Kikundi.
 2. Gusa maelezo ya kikundi.
 3. Weka maelezo mapya, kisha gusa Hifadhi.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La