Jinsi ya kutumia ujumbe wa salamu

Ujumbe wa salamu ni ujumbe unaoweza kubadilishwa unaotumwa kiotomatiki kwa wateja wako wanapokutumia ujumbe wa kwanza au wakati wowote wanapokutumia ujumbe baada ya siku 14 za kutokuwa na shughuli kwenye soga zao na wewe. Washa ujumbe wa salamu ili utagusane na wateja wako kiotomatiki kwenye mazungumzo.
Dokezo la Biashara: Weka ujumbe wa salamu kama vile “Habari! Nikusaidieje leo?” ili uwashirikishe wateja wako katika mazungumzo na kuwasaidia kujisikia wamekaribishwa. Hii inaweza kusababisha kuridhika kwa mteja.
Kuweka ujumbe wa salamu
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa Chaguo zaidi
  > Zana za Biashara > Ujumbe wa salamu.
 3. Washa Tuma ujumbe wa salamu.
 4. Gusa Ujumbe wa salamu ili kuhariri ujumbe wako wa salamu, kisha gusa SAWA.
 5. Gusa Wapokeaji halafu uchague mojawapo ya zifuatazo:
  • Kila mtu: kutuma kwa kila mtu anayekutumia ujumbe.
  • Kila mtu asiye kwenye kitabu cha anwani: kutuma kwa wateja wasio kwenye kitabu chako cha anwani.
  • Kila mtu isipokuwa…: kutuma kwa wateja wote isipokuwa wale uliowachagua.
  • Tuma tu kwa…: kutuma tu kwa wateja unaowachagua.
 6. Gusa HIFADHI.
Kumbuka: Lazima kifaa chako kiwe na muunganisho wa intaneti ili kutuma ujumbe wa salamu.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La