Jinsi ya kunyarakisha au kutoa nyarakani soga au kikundi

Kipengele cha kunyarakisha kinakuruhusu kuficha soga za kibinafsi au kikundi kutoka kwa orodha yako ya soga ili kupangilia vizuri mazungumzo yako. Unaweza kutazama soga zako zilizonyarakishwa kwa kuenda chini ya orodha ya Soga.
Dokezo:
  • Kunyarakisha soga ya kibinafsi au kikundi hakutafuta soga au kikundi.
  • Kunyarakisha soga zote za kibinafsi au kikundi kwa mara moja hakuwezeshwi kwenye KaiOS.
  • Soga ya kibinafsi au kikundi iliyonyarakishwa itatoka nyarakani unapopokea ujumbe mpya kutoka kwenye hiyo soga ya kibinafsi au kikundi.
Nyarakisha soga ya kibinafsi au kikundi
  1. Kwenye orodha ya Soga zako, chagua soga ya kibinafsi au ya kikundi unayotaka kunyarakisha.
  2. Bonyeza Hiari > Nyarakisha > SAWA.
Toa nyarakani soga ya kikundi au kibinafsi
  1. Elekea chini ya orodha ya Soga kwa kubonyeza kitufe cha chini > Nyarakisha soga.
  2. Chagua soga ya kibinafsi au kikundi unayotaka kuitoa nyarakani.
  3. Bonyeza Hiari > Toa Nyarakani > SAWA.
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kunyarakisha au kutoa nyarakani soga au kikundi: Android | iPhone | Web na Desktop
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La