Matumizi yasiyoidhinishwa ya ujumbe wa kiotomatiki au mwingi kwenye WhatsApp

WhatsApp ni jukwaa la kutuma ujumbe kwa faragha lililobuniwa ili kuwasaidia watu kuwasiliana na marafiki na wapendwa wao. Baada ya muda tumeona jinsi watu wanavyothamini kuwasiliana kwa ujumbe na biashara na kwa hivyo tumeunda zana mbili, programu ya WhatsApp Business na Jukwaa la WhatsApp Business, ili kuzisaidia kampuni kudhibiti mtagusano na wateja. Bidhaa zetu hazikusudiwi kutuma ujumbe mwingi au kiotomatiki, vyote ambavyo kwa kawaida vimekuwa ukiukaji wa Masharti yetu ya Huduma.
Tumejitolea kuimarisha hali ya faragha ya jukwaa letu na kuhakikisha usalama wa watumiaji wetu dhidi ya matumizi mabaya. Hivi majuzi tulieleza kwa kina uwezo wa jukwaa letu kutambua na kupiga marufuku akaunti katika waraka huu rasmi. Tunafahamu kuwa baadhi ya kampuni hujaribu kukwepa mifumo yetu ya mashine kujifunza, hata tunapojitahidi kuiboresha. Kwa kutumia taarifa za kiwango cha jukwaa zinazopatikana kwenye WhatsApp tumegundua na kuzuia mamilioni ya akaunti za unyanyasaji zisitumie huduma yetu.
Hii ni changamoto ambayo inahitaji mbinu kamili na WhatsApp imejitolea kutumia rasilimali zilizopo ikiwa ni pamoja na hatua za kisheria kuzuia unyanyasaji unaokiuka Masharti yetu ya Huduma, kama vile utumaji ujumbe wa kiotomatiki au mwingi au matumizi yasiyo ya binafsi. Hii ndiyo sababu pamoja na utekelezaji wa teknolojia, tunachukua pia hatua za kisheria dhidi ya watu binafsi au kampuni ambazo tuna ushahidi wa kwenye jukwaa kuhusu unyanyasaji kama huo. WhatsApp ina haki ya kuendelea kuchukua hatua za kisheria katika hali kama hizo.
Zaidi ya hivyo, kuanzia tarehe 7 Desemba, 2019, WhatsApp itachukua hatua za kisheria dhidi ya wale tunaoamua kuwa wanahusika na au wanawasaidia wengine katika unyanyasaji unaokiuka Masharti yetu ya Huduma, kama vile kutuma ujumbe wa kiotomatiki au mwingi au matumizi yasiyo ya binafsi, hata kama uamuzi huo umetokana na taarifa ambazo zinapatikana nje ya jukwaa letu pekee. Kwa mfano, taarifa za nje ya jukwaa zinajumuisha madai ya umma kuhusu uwezo wa kampuni kutumia WhatsApp kwa njia zinazokiuka Masharti yetu. Hii ni ilani kwamba tutachukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ambazo tuna ushahidi wa nje ya jukwaa kuhusu unyanyasaji, ikiwa unyanyasaji huo utaendelea baada ya tarehe 7 Desemba, 2019 au ikiwa kampuni hizo zinahusishwa na ushahidi wa unyanyansaji ulio kwenye jukwaa letu kabla ya tarehe hiyo.
Hakuna chochote katika tangazo hili kinapunguza haki ya WhatsApp kutekeleza Masharti yake ya kutumia teknolojia, kama vile kupiga marufuku akaunti kwa kutegemea uainishaji unaotokana na mashine kujifunza, WhatsApp itaendelea kufanya hivyo.
Tutaendelea kutoa uwezo wa kusaidia biashara kuwasiliana na wateja wao. Kw maelezo zaidi kuhusu uwezo kama huo, tembelea Programu ya WhatsApp Business na kurasa za Jukwaa la WhatsApp Business.
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La