Â
Jinsi ya kutumia kipengele cha bofya kupiga soga
Kipengele cha WhatsApp cha bofya kupiga soga kinakuruhusu kuanzisha soga na mtu bila namba ya mtu huyo kuhifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako. Ilimradi unajua namba ya simu ya mtu huyu na ana akaunti ya WhatsApp inayofanya kazi, unaweza kuunda kiungo kitakachokuwezesha kupiga soga naye. Kwa kubofya kiungo, soga na mtu huyo hufunguka kiotomatiki. Kipengele cha bofya kupiga soga kinafanya kazi kote kwenye simu yako na WhatsApp Web.
Kuunda kiungo chako
Tumia
https://wa.me/<number>
ambapo <number>
ni namba kamili ya simu katika muundo wa kimataifa. Ondoa sufuri zozote, mabano au vistari unapoweka namba ya simu katika muundo wa kimataifa.
Mifano:
Tumia:
https://wa.me/1XXXXXXXXXX
Usitumie:
https://wa.me/+001-(XXX)XXXXXXX
Kuunda kiungo chako ukitumia ujumbe ulioandaliwa mapema
Ujumbe ulioandaliwa mapema utaonekana kiotomatiki katika sehemu ya ujumbe kwenye soga. Tumia
https://wa.me/whatsappphonenumber?text=urlencodedtext
ambapo whatsappphonenumber
ni namba kamili ya simu katika muundo wa kimataifa na urlencodedtext
ni ujumbe uliojazwa awali uliosimbwa na URL.
Mfano:
https://wa.me/1XXXXXXXXXX?text=I'm%20interested%20in%20your%20car%20for%20sale
Kuunda kiungo kutumia ujumbe uliojazwa mapema, tumia
https://wa.me/?text=urlencodedtext
Mfano:
https://wa.me/?text=I'm%20inquiring%20about%20the%20apartment%20listing
Baada ya kubofya kiungo, utaonyeshwa orodha ya anwani unazoweza kuzitumia ujumbe.
Jinsi ya kutumia kitufe cha Soga kwenye WhatsApp
Kitufe cha Soga kwenye WhatsApp chenye chapa hufuata mwongozo wa chapa. Kwa kufuata miongozo ya chapa, kitufe hiki kitatambulika na kuaminiwa na wateja watarajiwa ambao wangependa kuwasiliana na wewe. Kitufe cha Soga kwenye WhatsApp kinapatikana katika rangi ya kijani na nyeupe na kwa ukubwa tofauti: ndogo, wastani na kubwa.
Ifuatayo ni mifano miwili ya jinsi kitufe rasmi cha Soga kwenye WhatsApp kinavyoonekana:
Kumbuka: Kwa sasa kitufe cha Soga kwenye WhatsApp kinapatikana kwa Kiingereza pekee.
Ili kuongeza mtagusano kutumia kitufe cha Soga kwenye WhatsApp, fuata hatua hizi bora:
- Tumia kitufe kama kilivyo. Usibadilishe kitufe.
- Tumia toleo la hivi karibuni la kitufe. Unaweza kupakua miundo ya kitufe hapa.
- Hakikisha kitufe kinaonekana na kinasomeka kwa urahisi.
Unaweza kutumia kitufe hicho cha Soga kwenye WhatsApp katika sehemu nyingi kama vile:
- kurasa za kutua kwenye vivinjari vya kompyuta
- kurasa za anwani
- programu za vifaa vya mkononi
- matoleo ya wavuti yako kwenye vifaa vya mkononi
- violezo kutoka kwa wasanidi wa wahusika wengine
Mifano ya msimbo wa HTML
- kupachika picha ya SVG:
- kupachika picha ya PNG
<a aria-label="Chat on WhatsApp" href="https://wa.me/1XXXXXXXXXX"><img alt="Chat on WhatsApp" src="WhatsAppButtonGreenLarge.svg" /><a />
<a aria-label="Chat on WhatsApp" href="https://wa.me/1XXXXXXXXXX"><img alt="Chat on WhatsApp" src="WhatsAppButtonGreenLarge.png" /><a />
Rasilimali zinazohusiana:
Jinsi ya kuongeza namba za simu za kimataifa