Kuhusu usajili na uhakiki wa hatua mbili

Unapofungua akaunti ya WhatsApp, utaona skrini mbili tofauti:
  • Usajili: Skrini hii huonekana unapofungua akaunti mpya au unaposajili tena akaunti yako iliyopo sasa. Kuthibitisha kwamba unamiliki hiyo nambari ya simu, utaulizwa kuingiza msimbo wa tarakimu 6 uliotumwa kwako kupitia SMS au simu. Kuthibitisha nambari yako ya simu kwa msimbo wa usajili ndiyo njia pekee unayoweza kuamilisha akaunti yako na ni lazima uweze kupokea msimbo kwenye simu yako.
  • Uhakiki wa hatua mbili: Skrini hii inaonekana baada ya kusajili nambari yako ya simu kwa ufanisi kwenye WhatsApp. Uhakiki wa hatua mbili ni kipengele cha hiari kinachoongeza usalama zaidi kwenye akaunti yako ya WhatsApp. Unapowezesha kipengele hiki, unaunda na kuthibitisha PIN ya kipekee inayohitajika kufikia akaunti yako. PIN ya uhakiki wa hatua mbili ni tofauti na msimbo wa usajili wa tarakimu 6 unaopokea kupitia SMS au simu. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu uhakiki wa hatua mbili kwenye makala haya.
Kama hukuwezesha uhakiki wa hatua mbili, lakini unaulizwa uingize PIN, mmiliki wa awali wa nambari ya simu anaweza kuwa aliiwezesha. Kwa hali hii, utahitaji kusubiri siku 7 kabla ya kuweka upya PIN ilikufikia akaunti yako.
Kama ukisahau PIN na umesajili nambari yako kwa ufanisi kwenye WhatsApp, gusa Umesahau PIN? > Lemaza kufikia akaunti yako.
Dokezo: WhatsApp inaweza kutumika tu kwa nambari moja ya simu kwenye kifaa kimoja kwa wakati mmoja. Baada ya kuisajili kwa ufanisi nambari yako ya simu kwenye WhatsApp, mtu yeyote anayeweza kuwa anatumia akaunti yako anaondolewa kiotomatiki na akaunti yako inakuwa imelindwa.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La