Â
Jinsi ambavyo historia yako ya utafutaji hushughulikiwa kwenye kipengele cha Gundua biashara
Android
Kipengele cha Gundua biashara hukusaidia kutafuta na kuwasiliana na biashara kwenye WhatsApp.
Unaweza kupata biashara kwa usalama, haraka na kwa urahisi kwa kufungua WhatsApp, kisha kugusa Biashara na kutumia chaguo za utafutaji wa HIVI KARIBUNI. Utafutaji wa HIVI KARIBUNI huorodheshwa chini ya kisanduku cha utafutaji. Unapoanza kuandika, chaguo za utafutaji wa HIVI KARIBUNI zitasasishwa pamoja na uorodheshaji wa biashara kulingana na herufi au maandishi yanayoandikwa kwenye kisanduku cha utafutaji.

Historia yako ya utafutaji itahifadhiwa kwenye simu yako pekee. Historia ya utafutaji hupatikana kwa siku 90 pekee kuanzia siku ambayo imetumiwa kwa mara ya mwisho, kabla ya kufutwa kabisa. Tafadhali kumbuka kuwa idadi ya utafutaji 50 pekee uliofanya hivi karibuni ndio utakaohifadhiwa na utafutaji huu wote utafikiwa chini ya utafutaji wa hivi karibuni.
Kufuta utafutaji wa hivi karibuni
- Ili kufuta utafutaji wako wa hivi karibuni, gusa FUTA YOTE.
- Gusa tena FUTA YOTE kwenye dirisha ibukizi la uthibitishaji.
- Historia yako ya utafutaji wa hivi karibuni itafutwa.
