Kuhusu vifaa vilivyounganishwa

Tumia WhatsApp kwenye Wavuti, Kompyuta na vifaa vingine kwa kuviunganisha na simu yako. Unaweza kutumia hadi vifaa vinne vilivyounganishwa na simu moja kwa wakati mmoja.
Ujumbe wako wa binafsi, maudhui na simu hufumbwa mwisho hadi mwisho. Kila kifaa kilichounganishwa huunganishwa na WhatsApp kivyake huku kikidumisha kiwango sawa cha faragha na usalama kupitia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho ambao watu wanaotumia WhatsApp wanautarajia.
Pata maelezo zaidi kuhusu ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye makala haya. Kwa maelezo ya jinsi tunavyokusanya, kuchakata na kushiriki data yako, tafadhali angalia Sera ya Faragha ya WhatsApp.
Kumbuka:
  • Si lazima simu yako iwe mtandaoni ili utumie WhatsApp kwenye vifaa vilivyounganishwa, lakini vifaa vyako vilivyounganishwa vitaondolewa ikiwa hutatumia simu yako kwa zaidi ya siku 14.
  • Utahitaji simu yako ili kusajili akaunti yako ya WhatsApp na kuunganisha vifaa vipya.
Vipengele visivyotumika
Vipengele hivi havitumiki kwa sasa:
  • Kuondoa au kufuta soga kwenye vifaa vilivyounganishwa ikiwa kifaa chako cha msingi ni iPhone.
  • Kutuma ujumbe au kupiga simu kwa mtu ambaye anatumia toleo la zamani sana la WhatsApp kwenye iPhone yake.
  • Kuangalia mahali mubashara kwenye vifaa vilivyounganishwa.
  • Kuunda na kuangalia orodha za matangazo kwenye vifaa vilivyounganishwa.
  • Kutuma ujumbe ulio na onyesho la awali la viungo kutoka kwenye WhatsApp Web.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La