Jinsi ya kutuma ujumbe wa sauti

Android
iPhone
KaiOS
Wavuti na Kompyuta ya dawati
Kama hutaki kuandika ujumbe, unaweza kunakili na kutuma ujumbe wa sauti.
Tuma ujumbe wa sauti
 1. Fungua soga ya kibinafsi au ya kikundi.
 2. Hakikisha sanduku la Ujumbe limechaguliwa.
 3. Bonyeza SAUTI > SAUTI na anza kuzungumza ili kunakili ujumbe wako wa sauti.
 4. Bonyeza Acha kuacha kunakili.
 5. Kisha unaweza:
  • Kubonyeza Cheza kusikiliza ujumbe wa sauti.
  • Kubonyeza TUMA kutuma ujumbe wa sauti.
  • Kubonyeza Futa kufuta ujumbe wa sauti.
Dokezo: Unaweza kusubiri kwa sekunde moja kabla ya kuzungumza kama mwanzo wa ujumbe wako haujanakiliwa.
Kwenye ujumbe wa sauti utaona:
 • Maikrofoni ya kijani
  kwenye ujumbe wa sauti ambao mpokeaji hajaucheza.
 • Maikrofoni ya bluu
  kwenye ujumbe wa sauti ambao mpokeaji ameucheza.
Dokezo: Video hapo chini inawahusu tu watumiaji wa WhatsApp ambao wana JioPhone au JioPhone 2.

Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La