Kutoweza kupiga simu kupitia kompyuta ya mezani

Wavuti na Kompyuta ya dawati
Windows
Ikiwa unakumbana na tatizo wakati wa kupiga au kupokea simu kwenye kompyuta ya mezani:
  • Hakikisha kuwa kompyuta na simu yako zimeunganishwa kwenye intaneti na kwamba una muunganisho thabiti wa intaneti.
  • Sasisha upate toleo jipya zaidi la WhatsApp.
  • Hakikisha kwamba kifaa chako kinaweza kupiga simu kwenye kompyuta ya mezani. Unaweza kupiga simu kwenye kompyuta ya mezani inayotumia mfumo wa Windows 10 64-bit toleo la 1903 au jipya zaidi na macOS 10.13 au jipya zaidi.
  • Hakikisha una maikrofoni, kamera, na spika.
  • Tatua hitilafu za maikrofoni na spika katika mipangilio ya sauti ya kompyuta yako.
  • Tumia vipokea sauti vinavyobanwa kichwani kwa sauti bora. Kutumia vifaa tofauti kwa ajili ya maikrofoni na spika kunaweza kusababisha mwangwi.
  • Hakikisha kamera yako inapatikana.
  • Hakikisha umetoa ruhusa ili WhatsApp ifikie maikrofoni na kamera yako.
Kumbuka:
  • Bado huwezi kupiga simu za vikundi kwenye WhatsApp Desktop kwa wakati huu.
  • Vifaa vya sauti na video pepe haviwezi kutumika.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La