Â
Jinsi ya kutuma midia, waasiliani au mahali
KaiOS
Unaweza kutuma emoji, midia, waasiliani au mahali katika ujumbe wa WhatsApp.
Tuma emoji, midia, waasiliani au mahali
- Fungua soga ya WhatsApp.
- Bonyeza +.
- Chagua unachotaka kutuma, kisha bonyeza:
- Emoji kuchagua na kutuma emoji.
- GIF kuchagua na kutuma GIF.
- Picha kupiga picha kwa Kamera yako au kuchagua picha kutoka kwenye Matunzio. Unaweza pia kuweka muhtasari kwenye picha yako.
- Video kurekodi video kwa Kamera yako au kuchagua Video kutoka kwenye simu yako. Unaweza pia kuweka muhtasari kwenye video yako.
- Sauti kutuma faili la sauti lililopo kutoka kwenye simu yako.
- Waasiliani kutuma maelezo ya waasiliani yaliyohifadhiwa kwenye kitabu cha anwani cha simu yako.
- Mahali kutuma mahali au eneo la karibu.
- Bonyeza Tuma.
Kumbuka: Upeo wa ukubwa wa mafaili yote ya picha, video na sauti unaoruhusiwa kutuma au kusambaza kupitia WhatsApp ni MB 10 kwenye simu zenye MB 512 na MB 5 kwenye simu zenye kumbukumbu ndogo.
Kuhifadhi midia
Kama unataka kuhifadhi midia unayopokea kwenye WhatsApp, bonyeza > Hiari > Mipangilio > Soga > Onyesha maudhui kwenye Matunzio. Picha na video zitahifadhiwa kwenye Matunzio na Video ya simu yako.