Jinsi ya kutumia lebo

Lebo hukusaidia kupanga na kupata soga na ujumbe wako kwa haraka. Unaweza kuunda lebo zenye rangi au majina tofauti, pia unaweza kuziongeza kwenye soga zote au katika ujumbe fulani kwenye soga.
Kuunda lebo
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa SOGA > Chaguo zaidi
  > Lebo.
 3. Gusa Ongeza > weka jina la lebo > gusa SAWA.
Kumbuka: Unaweza kuunda mpaka lebo 20.
Kuweka lebo kwenye soga
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa na ushikilie soga > gusa Lebo
  .
 3. Chagua lebo unayopenda > gusa HIFADHI.
Kuweka lebo kwenye ujumbe
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa na ushikilie ujumbe > gusa Chaguo zaidi
  > Weka ujumbe lebo.
 3. Chagua lebo unayopenda > gusa HIFADHI.
Kumbuka: Ikiwa lebo nyingi zinatumiwa kwenye soga au ujumbe, lebo zitaonekana moja juu ya nyingine.
Kutafuta maudhui yenye lebo
 1. Fungua programu ya WhatsApp Business.
 2. Gusa SOGA > Chaguo zaidi
  > Lebo.
 3. Gusa lebo.
Kutoka kwenye skrini ya Soga, unaweza pia kugusa picha ya jalada la mteja au aikoni ya kikundi ili uone lebo zote zinazohusishwa na soga hiyo.
Kudhibiti lebo
Gusa SOGA > Chaguo zaidi
> Lebo. Gusa lebo unayotaka kudhibiti. Unaweza kufanya mabadiliko yafuatayo:
 • Kuhariri lebo: gusa lebo > Chaguo zaidi
  > Hariri lebo.
 • Kubadilisha rangi ya lebo: gusa lebo hiyo > Chaguo zaidi
  > Chagua rangi.
 • Kufuta lebo: gusa lebo > Chaguo zaidi
  > Futa lebo > NDIYO.
 • Kuunda tangazo jipya: gusa lebo hiyo > Chaguo zaidi
  > Tuma ujumbe kwa wateja. Gusa alama ya tiki
  ili uandike na kutuma ujumbe wako.
  • Kumbuka: Ujumbe wa matangazo ulioundwa kwa kutumia lebo hauwezi kutumwa kwa vikundi. Wateja binafsi tu ndio watakaopokea ujumbe wa tangazo ulioundwa kwa kutumia lebo.
Dokezo la Biashara: Kuunda lebo za soga kama vile “Mteja mpya” na “Mteja anayerejea” hukusaidia kufuatilia mienendo ya matumizi ya wateja wako.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La