Jinsi ya kuunda jumbe zako
WhatsApp inaruhusu kuumba maandishi kwenye jumbe zako. Tafadhali zingatia, hamna hiari ya kuzima kipengele hiki.
Italiki
Kuweka italiki kwenye ujumbe wako, weka mstari pande zote mbili za maandishi:
_maandishi_
Herufi nzito
Kuweka herufi nzito kwenye ujumbe wako, weka nyota pande zote mbili wa maandishi:
*maandishi*
Mkato ulalo
Kuweka mkato ulalo kwenye ujumbe wako, weka kiwimbi pande zote mbili za maandishi:
~maandishi~
Nafasi moja
Kuweka
nafasi moja
kwenye ujumbe wako, weka alama tatu za kunukuu pande zote mbili za maandishi:```maandishi```
Kumbuka:
Mbadala, unaweza kutumia njia mkato kwenye Android na iPhone.
- Android: Gusa na shikilia maandishi unayo ingiza kwenye sehemu ya maandishi, kisha chagua Herufi nzito *, *Italiki *, au *Zaidi. Gusa Zaidikuchagua Mkato ulalo au Nafasi moja.
- iPhone: Gusa maandishi unayo ingiza kwenye sehemu ya maandishi > Chagua au Chagua Yote > B_I_U. Kisha, chagua Herufi nzito, Italiki, Mkato ulalo, au Nafasi moja.