Jinsi ya kuagiza ukitumia kikapu

Android
iPhone
Unapotembelea katalogi ya biashara, unaweza kutumia kitufe cha Tuma Ujumbe kwa Biashara ili uanzishe mazungumzo au tumia kitufe cha Ongeza kwenye Kikapu ili uanze mchakato wa kuagiza.
Kuongeza bidhaa kwenye kikapu
 1. Fungua WhatsApp.
 2. Nenda kwenye soga yako uliyotuma kwa biashara au jalada la biashara husika.
 3. Gusa aikoni ya kitufe cha ununuzi
  karibu na jina la biashara ili ufikie katalogi ya biashara hiyo.
 4. Vinjari bidhaa.
 5. Gusa
  karibu na bidhaa ili uongeze bidhaa hiyo kwenye kikapu chako. Unaweza pia kugusa bidhaa ili ufungue ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo. Gusa Ongeza kwenye kikapu.
  • Gusa
   au
   ili kuongeza au kupunguza idadi ya bidhaa hiyo kwenye kikapu chako.
Unaweza pia kugusa Tuma Ujumbe kwa Biashara ili kuuliza kuhusu bidhaa. Ili kuuliza kuhusu bidhaa nyingi, ongeza zote kwenye kikapu kisha utume maswali yako katika ujumbe mmoja. Oda haijakamilika hadi lithibitishwe na muuzaji.
Kubadilisha bidhaa zilizo kwenye kikapu chako
 1. Gusa Angalia Kikapu au
  kwenye menyu ya Katalogi au katika ujumbe kati yako na biashara ili uone bidhaa zilizoongezwa kwenye kikapu chako.
 2. Gusa Ongeza zaidi kurudi kwenye katalogi ili uendelee kuongeza bidhaa zaidi.
 3. Gusa
  au
  ili kuongeza au kupunguza bidhaa mahususi kwenye kikapu chako.
Kuagiza
 1. Baada ya kusasisha kikapu chako, gusa kitufe cha Agiza ili kutuma kikapu chako kwa muuzaji.
 2. Baada ya kutuma, unaweza kuona maelezo ya oda yako kwa kugusa kitufe cha Angalia kikapu katika dirisha la soga kati yako na muuzaji.
Rasilimali zinazohusiana:
Je, hili linajibu swali lako?
Ndiyo
La